Kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1999, ardhi yote ipo chini ya umiliki wa jumuiya, na itabaki chini ya usimamizi wa Rais kama mdhamini kwa niaba ya raia wote wa Tanzania. Sheria inatambua aina tatu ya ardhi ndani ya Tanzania ambazo ni ardhi ya jumla, ardhi ya kijiji na ardhi ya hifadhi.
Ardhi ya jumla ni ardhi ambayo imepimwa na ni ile iliyopo maeneo ya kandokando ya miji ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Ardhi yakijiji: hii ni ardhi iliyopo vijijini katika vijiji vya Tanzania. Baadhi ya vijiji vimepima ardhi yake ila kwa ujumla vijiji vingi havijafanya upimaji wa ardhi. Ardhi ya kijiji haiwezi kutumiwa kwa minajili ya uwekezaji hadi itakapobadilishwa kuwa ardhi ya jumla kupitia kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC).
Ardhi ya Hifadhi: ardhi hii hujumuisha hifadhi ya misitu, mbuga za wanyama na sehemu za burudani kwa ajili ya jumuiya. Endelea mwenyewe hapo chini
Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
Anuani ya Posta: S.L.P 686 MPANDA
Simu: +255759023788
Simu ya Kiganjani: 0759023788
Barua pepe: ded@mleledc.go.tz
Hakimiliki ya @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Hakizote zimehifadhiwa