HALMASHAURI YA WILAYA YA MLELE YADHAMILIA KUKUZA UCHUMI NA KUONGEZA KIPATO KWA HALMASHAURI NA KWA WANANCHI WAKE KWA KUWEKEZA KATIKA UJENGA WA KIWANDA CHA KUCHAKATA MAZAO YA NYUKI.
Ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele utakapokamilika utakuza uchumi na kuongeza kipato kwa wafugaji wa nyuki katika halmashauri ya Wilaya ya Mlele.
Ujenzi huo uko katika hatua ya ukamilishaji vitu vidogo vidogo kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 85 ya ujenzi na gharama za ujenzi wa mradi huo ni zaidi ya shilingi milioni 260 ujenzi wa huu ungharana fedha na fedhaa za Serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Comred Juma Zuberi Homera lifanya ziara kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo,ikiwa ni nyumba za watumishi,jengo la utawala, Kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki pamoja na jengo la akina mama na watoto.
Mkuu wa Mkoa Mhe Homera baada ya ukaguzi wa jengo la Kiwanda cha kukusanya,kufungasha na kuchakata mazao ya nyuki amesisitiza ukamilishaji wa kazi zilizosalia zikamilike ili kiwanda kianze kufanya kazi na tija ianze kuonekana ,kisha akapongeza kwa kazi nzuri inayoendelea ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo,na kuwataka wakamilshe mapema ili kiwända kiänze kufanya kazi.
Ameeleza kuwa soko la asali lipo siyo la kutafuta kiwanda kitasaidia kuchakata mazao ya nyuki tutapa nta na asali safi nasoko liko wazi jambo la Msingi amesistiza kukamilka mapema ili tija iweze kuonekana na mabidiliko yaweze kuonekana.
FURSA ZA UWEKEZAJI HALMASHAURI YA WILAYA MLELE.
Halmashauri ya Wilaya ya Mlele ina fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta za kilimo, mazao ya mistu nyuki,Utalii na mali Asili.
Bidhaa mbalimbali kutoka kwawajasiliamali ambazo ni pamoja na Asali ya nyuki wakubwa na wadogo,Mafuta ya Alzeti,bidhaa mbalmbli za mbao (Samani) watu wanakaribishwa kuchangamkia fursa za hizi za uwekezaji.
Halmashauri ya Wilaya Mlele ina utajiri mkubwa wa ardhi iliyozungukwa na mistu wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza Mlele hivyo ili kuweza kuchangia katika kutoa ajira na mapato kwa Serikali na Hälmashauri.
Yapo maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya wafugaji wakubwa,wakati na wadogo,hivyo wawekezaji wa ngazi zote mnakaribishwa kuja kuwekeza Mlele.
Kwenye sekta ya kilimo asilimia 87 ya kazi Halmashauri ya Wilaya Mlele wanategemea kilimo na ufugaji ndiyo huchangia kwa kiwango kikubwa cha uchumi wa Halmashauri ya Wilaya Mlele.
Halmashauri ya Wilaya ya Mlele yenye wakazi wapatao 56,695 kwa mjibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Halmashauri inundwa na Tarafa moja ya kiutawala,Kata sita,Vijiji 18,na Vitongoji 84 Wilaya inakadiliwa kuwa na jumla ya eneo lenye ukubwa wa hekta 698,102 Eneo linalofaa kwa kulima linakadiliwa kuwa ni hekta147,694 Jumla ya hekta ndizo zinazotumika kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na bustani mbogamboga na matunda.
Halmashauri ya wilaya ina wastani wa Joto sentgradi ya nyuzi 26 hupata aina moja ya mvua zenye kati ya milimita 920-1,200 kwa mwaka.
Msimu wa mvua huanza mwishoni mwa mwezi oktoba hadi Mwezi April na kipindi cha mvua nyingi ni kati y Januari hadi Machi,yapo maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji,wawekezaji wanakaribishwa.
Mazao mbalimbali ya chakula na biashara yanastawi vizuri ndani ya Halmashauri ambayo ni pamoja na mahindi,maharage,mihongo,migomba,karanga, viazi vitamu,viazi mvilingo,mihogo,alzeti,mpunga,pamba,tumbaku,korosho, ufuta,kunde na migomba.
Kwa upande wa Maliasili naUtalii Halmashauri ya Wilaya Mlele ni moja kati ya Halmashauri zenye maeneo yaliyosheheni Rasilimali muhimu kwa Utalii.Maliasili zilisheheni ni mtawanyiko wa mimea,mistu na wanyama mbalimbali pamoja na sehemu zenye mali kale.Kihistoria maumbile ya kuvutia ya milima yenye uoto wa asili.
Fursa za utalii ,
Biashara ya uwindishaji kitalii inafanyika Mlele kama njia ya uvunaji endelevu wa wanyampori,kama uwepo wa wanyama wa aina mbalimbali, kama twiga mweupe mnyama wa kipekee katika Ikolojia ya Hifadhi ya Katavi na maeneo ya Vitalu vya uwindaji.
Kuna uoto pekee uliosheheni mistu ya miombo na mining,maeneo ya kihistoria na matambiko ya machifu,Mlele imeunganishwa na barabara ya lami kutoka Tabora kwenda makao makuu ya Mkoa Mjini Mpanda na maeneo mengine, uwepo wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda na ujenzi wa Bandari ya kisasa Karema inayounganisha nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC ni moja ya fursa muhimu ya kiuchumi.
Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
Anuani ya Posta: S.L.P 686 MPANDA
Simu: +255759023788
Simu ya Kiganjani: 0759023788
Barua pepe: ded@mleledc.go.tz
Hakimiliki ya @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Hakizote zimehifadhiwa