Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera anaeleza fursa za Uwekezaji zilizopo katika Mkoa wa Katavi wakati wa Uzinduzi wa Mwongozo wa kitabu cha Uwekezaji Mkoani Katavi, Hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mpanda Manispa Hall, Machi 3’ 2021
Mkoa wa Katavi umezindua kitabu cha Mwongozo wa uwekezaji ili kutoa uelekeo wa uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani ya nchi na nje Kitabu ambacho kitakuwa mwongozo wa kuwaongoza wawekezaji ambao wana karibishwa kuja kuwekeza.
Kuzinduliwa kwa kitabu hicho kutasaidia katika kuweka mwelekeo mzuri wa kuonesha wapi wawekeze ambapo mkoa umeainisha maeneo ya uwekezaji katika sekta mbalimbali ziwe za kilimo,utalii,Biashara ujenzi wa viwanda.
Kuzinduliwa kwa kitabu hicho kutaleta mafanikio gani kwa jamii ya wanakatavi na Taifa kwa ujumla,zaidi ya miaka kumi iliyopita kuliwahi kufanyika kongamano la uwekezaji kwa Mikoa ya Ukanda Ziwa Tanganyika iliyojumuisha mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa huku Mkoa wa Tabora ukikaribishwa kama mwalikwa.
Tangu kuwepo kwa kongamano hilo kumekuwepo mabadiliko mbalimbali,katika sekta za kiuchumi kiutamaduni na Nyanja nyingine za kijamii.
Wawekezaji waliopata nafasi kushiriki katika Kongamano la uzinduzi wa Kitabu cha muongozo wa uwekezaji mkoani Katavi wamehimizwa kuchangamkia fursa za uwekezaji katika mkoa huo wenye zaidi ya hekta 45,000.
Akizungumza katika mkutano huo uliowakutanisha wadau wa uwekeaji kutoka maeneo mbalimbali, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera ameeleza kuwa katika ujenzi wa viwanda Mkoa umetenga hekari 245 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda mbalimbali.
“Kutokana na wingi wa samaki wanaovuliwa kutoka ziwa Tanganyika wakiwemo, migebuka, kuhe, sangara pamoja na kamongo, Mkoa umetenga hekari 245 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya kusindika na kuchakata samaki” kwa mjibu wa Mkuu huyo wa Mkoa Mhe, Homera
Mkuu huyo wa Mkoa ameongeza kuwa wawekezaji wanayo fursa ya ujenzi wa viwanda mbalimbali vikiwemo viwanda vya usindikaji nafaka, ujenzi wa viwanda vya asali, uchakataji wa nyama na maziwa, pamoja na viwanda vya mbao.
Katika sekta ya utalii Mkuu wa Mkoa Homera amesema wawekezaji wanayofursa ya kuwekeza, kwa upande wa makampuni ya utalii yatakayosaidia ongezeko la utalii katika Mkoa huo, wenye vivutio vingi vva utalii ikiwemo mto mapacha wenye maji yanayosadikika kuwa ukiyanywa maji hayo unazaa watoto mapacha,eneo la chemichemi ya maji moto pamoja na hifadhi ya Taifa Katavi yenye ukubwa wa hekari 4471 na ambayo inawanyama wakubwa kuliko maeneo mengine hapa nchini.
Mhe, Homera anasema kuwa hapa nanukuu “Tuna zaidi ya sokwe 2500, tuna twiga mweupe ambaye huwezi kumpata kokote Tanzania isipokuwa Mkoani katavi, lakini pia tunao Viboko na Tembo wakubwa sana kama nyumba” Anasema Mhe, Homera.
Mapema Prof Leonard Mwaikambo ambaye alihusika katika kuandaa na kuandaa andiko kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Katavi ameeleza taasisi ya kiuchumi ya kijamii wamekuwa wakibainisha vivutio vya uwekezaji.
Mpaka sasa Mikoa 17 imezindua mwongozo ukiwamo Mkoa wa Katavi,fursa kubwa za kilimo ufugaji na utalii,fursa zikitumika vizuri zitaboresha maisha ya wanajamii ya Mkoa wa Katavi na watanzania kwa ujumla.
Akizungumza katika Kongamano la uzinduzi wa Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji kwa niaba ya Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uwekezaji Prof, Kitila Mkumbo ameleza kufurahishwa na juhudi za Mkoa katika kuvutia wawekezaji kwa kuandaa mipango yao mizuri inayowavutia wawekezaji.
Prof Mkumbo amesema Mkoa wa Katavi ni muhimu kwa nchi yetu kwenye kilimo,madini na utalii na wana äkili ya uwekezaji.
Amesema Mfumo wa kiuchumi wa fedha duniani unahitaji watu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa bidii, mwekezaji ni lazima awe na pesa nyingi.
Wawekezaji wapo wa aina mbalimbali wa ndani na wa nje Serikali na wadau mbalimbali,kwa mantiki hiyo watumishi watambue kuwa wajibu wao ni kutengeneza mazingira mazuri ya wawekezaji.
Amesema wawekezaji wakifanikiwa ndipo serikali nayo inapopata mapato,katika kukuza uchumi nchi inahitaji wawekezaji.
Kwa mtumishi wa Serikali yeyote anayekwamisha wawekezaji anakwamisha mipango ya Serikali, Serikali na Serikli haitamuonea aibu itaßhughulika naye, na itawalinda wawekezaji ambao ni wazuri,.
Prof Mkumbo amesema ni jukumu la Mkoa kuwawesha wawekezaji na kazi ya wizara ikishirikiana na mikoa katika kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.
Mwongozo wa Serikali hawataki kuona wawekezaji wananyanyaswa,wawekezaji watimize wajibu wao kwa kufuata
sheria za nchi,ingawa wapo wachache wenye changamoto watapambanao kwa kufuata sharia.
Amemalizia kwa kueleza kuwa serikali inataka kuweka mwongozo namna wanavyoweza kuwekeza katika kuwakodisha na kuwahudumia na
Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
Anuani ya Posta: S.L.P 686 MPANDA
Simu: +255759023788
Simu ya Kiganjani: 0759023788
Barua pepe: ded@mleledc.go.tz
Hakimiliki ya @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Hakizote zimehifadhiwa