Tawala wa Wilaya ya Mlele Mhe Linkolin Tamba akimkabidhi mkulima miche ya korosho kwa ajili ya kupanda kwenye mashamba yao hafla iliyofanyika mjini Inyonya kilipo kitalu cha kuoteshea miche ya korosho iliyooteshwa na Halmashauri na kugawiwa bure kwa wakulima katika vijiji vyote 18 katika Halmashauri hiyo ambapo zaidi ya miche 53 imeoteshwa.
Kilimo cha korosho ni moja ya mazao ya kimkakati katika halmashauri na mkoa wa Katavi iwapo wakulima watazingatia ushauri w watalaam wa kilimo zao hilo linawez kbadilisha uchumi wa wananchi hao na kuingizia pato halmashauri na Täifa kwa ujumla.
Halmashauri ya wilaya ya Mlele ni moja ya Halmashauri tano katika mkoa wa Katavi zenye maeneo ya ardhi yenye rutuba na kila aina ya mazao yanastawi,ina mistu ya kutosha aina ya miyombo ambayo inafaa kwa ufugaji wa nyuki na kila aina ya rasilimali.
Mbali ya kilimo cha zao la korosho pia wananchi wanalima pamba,alzeti,ufuta ambayo nayo ni mazao ya kimkakati pamoja na kilimo cha mazao ya chakula na biashara mahindi,mpunga,mihogo na karanga.
Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
Anuani ya Posta: S.L.P 686 MPANDA
Simu: +255759023788
Simu ya Kiganjani: 0759023788
Barua pepe: ded@mleledc.go.tz
Hakimiliki ya @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Hakizote zimehifadhiwa