KIPINDI CHA PILI CHA AWAMU YA TATU YA TASAF
Madhumuni na muda wa utekelezaji
•Madhumuni ya Mpango wakati wa Kipindi cha Pili ni kuwezesha kaya za walengwa kutumia fursa za kuongeza kipato na huduma za jamii na uchumi na kuwekeza katika kuendeleza watoto wao.•Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF kinatekelezwa kuanzia mwaka 2020 hadi 2023.
Eneo la Utekelezaji wa Mpango.
•Utekelezaji utafanyika kwenye Mamlaka za Maeneo ya Utekelezaji 187 (Halmashauri 185 za Tanzania Bara na Unguja na Pemba, Zanzibar • •Ikiwa ni pamoja na asilimia 30 ya vijiji/mitaa/shehia ambazo hazikufikiwa kwenye utekelezaji wa Kipindi cha Kwanza na kuandikisha kaya maskini sana kwenye vijiji/mitaa/shehia za Kipindi cha Kwanza, ambazo hazikuwa zimeandikishwa.
Msisitizo wa Kipindi cha Pili.
i.Kuwezesha kaya kufanya kazi na hivyo kuongeza kipato,ii.Kuwezesha kaya za walengwa kuongeza rasilimali zalishi na kuongeza vitega uchumi,iii.Kuwekeza katika rasilimali watu hususan watoto ili kuleta matokeo chanya yatakayodumu kwa muda mrefu,iv.Kuboresha upatikanaji wa huduma za maji, afya na elimu, Kukuza uchumi wa eneo unakofanyika utekelezaji kutokana na matokeo ya Mpango
Sehemu za Mpango
Programu za Jamii
i.Uhawilishaji fedha: ruzuku kwa kaya zenye watoto, kaya zenye wenye ulemavu na kaya zenye watoto wa kutimiza masharti ya elimu na afyaii.Miradi ya Kutoa Ajira ya Muda kwa walengwa ikihusisha kuendeleza miundombinu mahsusi ya Afya, Elimu na Majiiii.Kukuza uchumi wa kaya
II. Kuimarisha Taasisi na Mifumo
PROGRAMU ZA JAMII
UHAWILISHAJI FEDHA
•Ruzuku kwa kaya ambazo hazina wanakaya wenye uwezo wa kufanya kazi.•Ruzuku kwa kaya zenye wanakaya wenye ulemavu - kwa kutambua changamoto na gharama zinazoongezeka kwa kuishi na wanakaya mwenye ulemavu.•Ruzuku kwa kaya zenye watoto walio shuleni na wale wa chini ya miaka mitano.•Ruzuku kwa kaya kuhawilishwa kwa njia za kielektroniki.
Viwango vya malipo ya ruzuku
Aina ya ruzuku
|
Ruzuku
|
Kiasi (TZS)
|
Maelezo
|
Kiwango cha Juu (TZS)
|
Kiwango cha msingi
|
Ruzuku ya msingi
Yenye manufaa |
12,000
|
Kuandikishwa kwenye Mpango
|
12,000
|
Kiwango cha msingi
|
Ruzuku ya kuwa na watoto
|
5,000
|
Chini ya miaka 18
|
5,000
|
Kiwango cha msingi
|
Watoto
|
5,000
|
Miaka 0-5 Afya
|
5,000
|
Inayobadilika
|
Shule ya msingi (1-4)
|
2,000
|
Shule ya msingi
|
12,000
|
Inayobadilika
|
Shule ya msingi (5-7)
|
4,000
|
Shule ya msingi
|
|
Inayobadilika
|
Shule ya sekondari (1-4)
|
6,000
|
Shule ya sekondari
|
16,000
|
Inayobadilika
|
Shule ya sekondari (5-6)
|
8,000
|
Shule ya sekondari
|
|
Kiwango cha msingi
|
Wenye ulemvu
|
5,000
|
Wenye ulemvu
|
5,000
|
Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
Anuani ya Posta: S.L.P 686 MPANDA
Simu: +255759023788
Simu ya Kiganjani: 0759023788
Barua pepe: ded@mleledc.go.tz
Hakimiliki ya @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Hakizote zimehifadhiwa