• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watuishi |
Mlele District Council
Mlele District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Msingi Mkuu
    • Mpango Mkakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Maji
        • Historia
        • Dhima na Dira
        • Muundo wa Taasisi
        • Ukaribisho
        • Jaribu
        • what we do
        • Huduma ya Maji
        • Huduma za Afya
        • Elimu Msingi
        • Huduma
        • Mwenyekiti wa Halmashauri
        • Mkurugenzi Mtendaji
        • Utawala na Rasilimali watu
        • /TEHAMA-na-Takwimu
        • Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii
        • Mipango takwimu na Ufuatiaji
        • Ardhi na Maliasili
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Sheria
        • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Maendeleo ya Jamii
        • Idara
        • Vitengo
        • Ujenzi
        • Maji
        • Ugavi na Manunuzi
        • Usafishaji na Mazingira
        • Uchaguzi
        • Tasaf III
        • Mainstreaming Sustainable Forest Managment in Woodland of Western Tanzania Project
        • Mwenge waUhuru
        • UKIMWI/ VVU
        • Risk Oficer Cordinator
        • Miradi inayoendelea
        • Zabuni
        • Kazi za Idara Utumishi
        • Muundo wa Halmashauri
        • Miradi Lengwa
        • Kitengo cha nyuki
        • Mwenge
        • Sera ya Faragha
        • Kanusho
        • Machapisho
        • Sheria
        • MTF
        • Fomu
        • Orodha ya Madiwani
        • Fedha, Uongozi na Mipango
        • UKIMWI
        • Maji
        • Mipango Miji na Mazingira
        • Uchumi, Afya na Elimu
        • Maadili
        • Ratiba
        • Vikao vya waheshimiwa
        • Kuonana na Mwenyekiti
        • Madiwani
        • Kanausho
        • Huduma ya Maji
        • Huduma ya Afya
        • Huduma ya Kilimo
        • Huduma ya Elimu
        • Huduma ya Ufugaji
        • Huduma za Uvuvi
        • Huduma za Sheria
        • Huduma za kiutumishi
        • Vivutio vya Utalii
        • Kilimo
        • Ufugaji
        • Itakayo tekelezwa
        • Inayoendelea
        • Iliyo Tekelezwa
        • muongozo
        • Sheria Ndogo
        • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
        • Mpango Mkakati
        • Taarifa
        • Fomu Mbalimbali
        • Taarifa kwa Umma
        • Video za shughuli zetu
        • Maktaba ya Picha
        • Magazeti
        • Hotuba
        • ORODHA YA WAJUMBE WA KAMATI MBALIMBALI ZA KUDUMUKWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020
        • KARENDA YA VIKAO VYA KISHERIA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA MLELE KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya
    • Viengo
      • Kitengo cha TEHAMA na Mahusiano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Uchaguzi Uchaguzi
      • Kitengo cha nyuki
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Huduma za Kilimo
    • Uvuvi
    • Elimu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orotha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Mazingira
      • UKIMWI
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa
      • Kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Mkataba wa Huduma
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
  • Kiini cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Album ya Picha
    • Video
    • Hotuba
  • TASAF

eneo la mizani kijiji cha kamsisi

Posted on: September 22nd, 2022

Eneo ilipojengwa Mizani Kata ya Kamsisi kama linavyoonekana Mwonekano wake, Barabara ya lami iliyojengwa kutoka Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi kuelekea Mkoa wa Tabora ambayo inafungua fursa za kiuchumi ikitumiwa vyema na wakazi wa Mkoa wa Katavi itakuwa mkombozi kwao. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.)

4.MAKALA YA FURSA ZA KIUCHUMI MLELE.

Kufunguka kwa  barabara  za  Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi zilizojengwa kwa kiwango cha lami, kunachochea maendeleo na  kunasaidia kutokomeza umasikini miongoni mwa wakazi wa wilaya hiyo na mkoa wa Katavi kwa ujumla.

Hii ni Kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe.Filberto Sanga  ambaye anawatia moyo wakazi wa hao kutumia fursa hiyo kuanza kubadilisha maisha yao.

Halmashauri ya wilaya ya Mlele ina watu wenye uwezo Mkubwa  kifedha  na wana mwamko mkubwa katika kuchapa  kazi na watu wenye uwezo  wa kumiliki  mashirika na Taasisi mbalimbali waje wanakaribishwa kuja Mlele kuwekeza  kusudi wananchi waweze kupata huduma zote muhimu  badala ya kuzifuata   nje ya wilaya anasema Sanga

 Kihistoria Mlele ni miongoni mwa wilaya  yenye fursa nyingi za kiuchumi,kuboreshwa kwa miundombinu ya barabara ni wazi kunafungua fursa zaidi kwa wawekezaji hasa wafanyabiashara  wadogo na wakubwa kutoka ndani na nje ya wilaya kuwekeza katika sekta mbalimbali zikiwemo za viwanda,madini,kilimo,na utalii.

Ardhi wilayani humo ina rutuba ya kutosha  na inaruhusu kulima mazao ya aina mbalimbali’.

Nawakaribisha wawekezaji wa ndani na nje wasisite kuja huku,ile mikingamo ya ubovu wa barabara sasa haipo tena.

Tunahitaji na sisi tuwe angalau na maduka makubwa ya kisasa yatakayouza bidhaa mbalimbali.

Ujio wa barabara hizi pia unasaidia hata sisi kusafiri na siyo kusafirisha mazao tu,sasa tunasafiri kirahisi kutoka sehemu moja  kwenda nyingine  barabara hizi zinasaidia wananchi kujifunza mambo mengi yafanywayo na wenzetu maeneo mengine.

Wilaya ya Mlele ni sehemu yenye mzunguuko mkubwa wa fedha kulingana na mazingira yake kilichokuwa kinakwamisha ni barabara za uhakika.

Kujengwa kwa barabara kwa kiwango cha lami kumesaidia kufungua pande zote za wilaya hiyo na Mkoa.

“Kwa sasa kwenda maeneo mengine kama Mpanda ,Sikonge Tabora mwanza, Arusha na Dar es Salaam imekuwa rahisi barabara hizo zote zimeunganisha miji mikubwa katika nchi na wilaya ya Mlele siyo kisiwa tena kama hapoa awali tulipokuwa hakuna barabara ya lami” anasema Mkuu wa Wilaya Sanga.

Mkuu wa Wilaya anatoa wito gani kwa wananchi wa wilaya ya Mlele?Anasema wakazi wa Mlele wazitumie Barabara hizo kujenga uchumi  imara hasa kwa sekta ya kilimo ambacho ni utii wa mgongo wa wilaya mkoa na Taifa kwa ujumla.

Shughuli zetu kubwa ni  kilimo na sisi tumeishatangazo kama wilaya ya kilimo kuwa mwaka huu mlele ina akiba ya chakula cha kutosha   hali hii inaonesha jinsi gani tunajitosheleza kwa chakula.

Mkuu wa Wilaya Mlele Mhe. Sanga anahimiza wazitumie barabara kama kichocheo cha maendeleo.

Pia anachukua fursa kuwapongeza wananchi kwa uchapakazi wao na siyo wavivu wanafanya kazi ,ziwe za kilimo,uvuvi, ufugaji na hata shughuli za biashara na ujasiliamali.

Wananchi wafanye kazi zitakazoinua uchumi kuanzia ngazi ya familia na taifa zitasaidia kuongeza kipato.

Akizungumzia uuzwaji wa mazao Mkuu wa Wilaya anasema Serikali inaposisitiza kilimo na uuzaji wa mazao,sikwamba kila mkulima anapaswa kuuza mazao yote, Hapana lazima aweke akiba ya chakula cha familia auze ziada.

Kuhusu maeneo ya uwekezaji Mhe.Sanga anasema Mlele inayo maeneo mengi ya uwekezaji wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika sekta  mbalimbali.

Naye Meneja wa wakala wa Barabara Tanzania Tanroad Mkoa wa Katavi Mhandisi Martin  Mwakabende anasema ujenzi wa barabara ya lami wilaya ya Mlele kwenda Sikonge Tabora umekamilika ambapo barabara hiyo inatoka Mpanda hadi Tabora iliyojengwa kwa kiwango cha lami imekamilika na ina urefu wa kilometa 196.sanjali na ujenzi wa daraja la Koga lenye urefu wa mita 120.

Kukamilika kwa ujenzi huo sasa kumefungua milango ya mawasiliano yenye uhakika kwa wananchi.

Awali haikuwa rahisi kutoka Mlele Katavi kwenda maeneo mengine kama Tabora lakini baada ya ya kukamilika kwa barabara kuna mabasi na magari  ya kawaida mengi yanatumia barabara hiyo na watu wengi sasa hivi  wanapenda kupita njia hiyo kwenda Tabora,Mpanda Mwanza Arusha na Dar es Salaam.

Je! kuna changamoto gani zilizopo hivi sasa Mhandisi Mwakabende anasema kila lenye jema halikosi changamoto, kufunguliwa  kwa barabara hizo kumeongeza idadi ya magari hivyo ajali za barabarani nazo zimeongezeka hasa za mabasi na malori.

Ajali hizo zinaharibu vyuma vilivyowekwa pembezoni mwa barabara,changamoto nyingine ni wezi na waharibifu wa alama za barabarani.

Pia kumekuwepo na raia wasio wema wanavunja na kuiba alama za barabarani hata hivyo mamlaka zinaendelea kuwafuatilia waharibifu wa kingo hizo wameanza kuchukua hatua ya udhibiti kwa kuwandikia chaji kwa ajili ya kurekebisha.

Changamoto nyingine ni elimu kwa wakazi wanaoishi jirani na barabara,watu wanaiba alama za barabarani kwa mfano lefrekta , wanaiba na kuzifunga kwenye baiskeri zao wanapashwa kupatiwa  elimu ili waache kuiba

.Changamoto nyingine ni shughuli za kilimo kwenye hifadhi ya barabara hii inapelekea maji kutawanyika na kusababisha tuta la barabara kubomoka pamoja na changamoto ya kumwaga mafuta na kupitisha mifugo barabarani inaharibu sana barabara.

Hata hivyo baadhi  ya wakazi wa Wilaya ya Mlele wanaishukuru serikali kwa kujenga barabara kwa kiwango cha lami Agostine  Mbalamwezi ni mmoja wa wananchi  wa Inyonga anasema kujenga barabara kwa kiwango cha lami zimerahisha shughuli za biashara na kuleta maedeleo ya haraka.

Hivi sasa wafanyabiashara wa Inyonga Mlele na Mkoa wa Katavi kwa ujumla wanafanya biashara zao maeneo ya wilaya nyingine na kurudi mfano wanaweza kuondoka asubuhi kwenda sikonge Tabora asubuhi jioni, wakarudi hilo ni jambo ambalo awali walilazimika kwenda siku moja kabla, kutokana na ubovu wa barabara.

Mbalamwezi anasema hali ilikuwa mbaya, kipindi cha nyuma tulilazimika kutumia siku nne hadi tano kusafirisha bidhaa zetu na kipindi cha masika tulikuwa tukipoteza muda mwingi fedha na hata ndoa zetu ziliyumba ,lakini sasa hali ni nzuri tunafurahi kuwa raia wa Tanzania ,alisema Mbalamwezi.

Naye Mama Msabaha na Mark Matandiko  wanasema wananchi watumie fursa hiyo kwenda kuwekeza wilaya ya mlele na Mkoa wa Katavi kwa ujumla hasa biashara ya viazi,mahindi karanga alzeti na mpunga mazao ambayo ni rahisi kusafirisha na yanapatikana kwa wingi katika mkoa huo.

Mzee Matandiko anasema kutokana na kukamilika kwa barabara ya lami hata biashara  ya nyumba za kulala wageni mahitaji yake yameongezeka,watu wanazidi kuja huku hata nyumba za kupangisha na ofisi zinahitajika mahitaji yameongezeka sana.

Halafu huku kuna hifadhi ya Taifa ya  Katavi na Mapori ya akiba,barabara hizi zitawaleta watalii wengi na wengine watahitajika kutembelea maeneo mbalimbali ya kitalii na kujionea vivutio vyetu.watu waje kuwekeza huku anasema Mama Msabaha na Mzee Matandikio kwa nyakati tofauti.

Bi Teresia Irafay ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele anasema kufunguka kwa barabara ya Mlele- Mpanda na Mlele Tabora kutahamasisha  ujengaji wa mahoteli na nyumba za kisasa za wageni kwani ardhi ipo ya kutosha.

Hata mapato ya Halmashauri yataongezeka kutokana na makusanyo ya mapato, kwa kuwa halmashauri ina viwanja kwa ajili ya matumizi mbalimbali vilivyopimwa.

Eneo lilipojengwa  jengo la utawala kuna viwanja vinauzwa vinahitaji waendelezaji halmashauri inatarajia kupata fedha kutokana na viwanja hivyo.

Mwezi mei tarehe 18 mwaka 2022  Mhe. Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya ufunguzi wa barabara ya Mpanda,Mlele Koga hadi Tabora yenye urefu wa kilometa 342.9 iliyokamilika kwa kiwango cha lami inayounganisha mikoa ya Katavi na Tabora.

Katika hotuba yake kwa wananchi aliyoitoa wilaya ya Sikonge aliwataka wananchi kuilinda barabara hiyo na kuwataka wafuate sheria zote za usalama zilizowekwa ili kuifanya barabara kudumu na kuongeza  usalama wa watu na mali zao huku akisisitiza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutapelekea kuongezeka kwa wawekezaji na kupanua uchumi  kwenye ukanda huo na nchi kwa ujumla.

Wito kwa wananchi waendelee kufurahia matunda ya serikali lakini watambue miundombinu inayotengenezwa ni kwa faida yao na vizazi vijavyo wanapaswa kuitunza hivyo wasisite kutoa taarifa sehemu husika wanapobaini mtu yeyote anayeharibu hasa kwa kung’oa kingo za barabara na alama zake. mwisho

Makala haya yameandaliwa na Kibada Ernest Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Mlele

Matangazo

  • TANGAZO KUTOKA TUME HURU YA UCHAGUZI March 03, 2025
  • MABADILIKO YA UKUMBI WA USAILI MLELE DC October 04, 2024
  • Tangazo la Ajira ya ukusanyaji wa Mapato July 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI MBALIMBALI ZA AFYA December 10, 2021
  • Waonaji wote

Habari Mpya

  • MIRADI YA MWENGE 2025

    July 01, 2025
  • SIKU YA WAJANE DUNIANI

    June 23, 2025
  • ZIARA YA MAFUNZO MANISPAA YA MOSHI {UKUSANYAJI WA MAPATO}

    June 19, 2025
  • ZIARA YA MAFUNZO MANISPAA YA MOSHI {UDHIBITI WA TAKA NGUMU}

    June 20, 2025
  • Waonaji wote

Video

#TBC LIVE ZOOM: YALIYOJIRI NA MAFANIKIO YA ZIARA YA RAIS SAMIA NCHINI QATAR
Video Zaidi

wavuti za Haraka

  • FACE BOOK PAGE YA MLELE
  • MLELE DC BLOG
  • kilimo na umwagiliaji
  • mafunzo tovuti za serikali kanda ya magharibi
  • MAONESHO
  • Tuma barua pepe hapa

Wavuti Mwambata

  • Wizara ya Utumishi wa Umma
  • Tume ya ajira ya Tanzania
  • Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania
  • Jamhuri ya muungano wa tanzania
  • Tawala za mikoa na Serikali za mitaa
  • BARAZA LA MITIHANI

Takwimu za Watembeleaji

world map hits counter

Hesabu Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele

    Anuani ya Posta: S.L.P 686 MPANDA

    Simu: +25525295197

    Simu ya Kiganjani: 0786077372

    Barua pepe: ded@mleledc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ya @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Hakizote zimehifadhiwa