• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watuishi |
Mlele District Council
Mlele District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Msingi Mkuu
    • Mpango Mkakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Maji
        • Historia
        • Dhima na Dira
        • Muundo wa Taasisi
        • Ukaribisho
        • Jaribu
        • what we do
        • Huduma ya Maji
        • Huduma za Afya
        • Elimu Msingi
        • Huduma
        • Mwenyekiti wa Halmashauri
        • Mkurugenzi Mtendaji
        • Utawala na Rasilimali watu
        • /TEHAMA-na-Takwimu
        • Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii
        • Mipango takwimu na Ufuatiaji
        • Ardhi na Maliasili
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Sheria
        • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Maendeleo ya Jamii
        • Idara
        • Vitengo
        • Ujenzi
        • Maji
        • Ugavi na Manunuzi
        • Usafishaji na Mazingira
        • Uchaguzi
        • Tasaf III
        • Mainstreaming Sustainable Forest Managment in Woodland of Western Tanzania Project
        • Mwenge waUhuru
        • UKIMWI/ VVU
        • Risk Oficer Cordinator
        • Miradi inayoendelea
        • Zabuni
        • Kazi za Idara Utumishi
        • Muundo wa Halmashauri
        • Miradi Lengwa
        • Kitengo cha nyuki
        • Mwenge
        • Sera ya Faragha
        • Kanusho
        • Machapisho
        • Sheria
        • MTF
        • Fomu
        • Orodha ya Madiwani
        • Fedha, Uongozi na Mipango
        • UKIMWI
        • Maji
        • Mipango Miji na Mazingira
        • Uchumi, Afya na Elimu
        • Maadili
        • Ratiba
        • Vikao vya waheshimiwa
        • Kuonana na Mwenyekiti
        • Madiwani
        • Kanausho
        • Huduma ya Maji
        • Huduma ya Afya
        • Huduma ya Kilimo
        • Huduma ya Elimu
        • Huduma ya Ufugaji
        • Huduma za Uvuvi
        • Huduma za Sheria
        • Huduma za kiutumishi
        • Vivutio vya Utalii
        • Kilimo
        • Ufugaji
        • Itakayo tekelezwa
        • Inayoendelea
        • Iliyo Tekelezwa
        • muongozo
        • Sheria Ndogo
        • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
        • Mpango Mkakati
        • Taarifa
        • Fomu Mbalimbali
        • Taarifa kwa Umma
        • Video za shughuli zetu
        • Maktaba ya Picha
        • Magazeti
        • Hotuba
        • ORODHA YA WAJUMBE WA KAMATI MBALIMBALI ZA KUDUMUKWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020
        • KARENDA YA VIKAO VYA KISHERIA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA MLELE KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya
    • Viengo
      • Kitengo cha TEHAMA na Mahusiano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Uchaguzi Uchaguzi
      • Kitengo cha nyuki
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Huduma za Kilimo
    • Uvuvi
    • Elimu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orotha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Mazingira
      • UKIMWI
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa
      • Kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Mkataba wa Huduma
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
  • Kiini cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Album ya Picha
    • Video
    • Hotuba
  • TASAF

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYA YA MLELE KATAVI

Posted on: August 7th, 2022




MAKAMU WA RAIS DK.MPANGO ATOA MAAGIZO MAZITO KWA WIZARA YA NISHATI







  

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini na Chama wakati alipowasili katika Uwanja wa Shule ya Msingi Inyonga Wilaya ya Mlele mkoani Katavi kuzungumza na wananchi.

  

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Dkt. Philip Mpango akicheza wimbo maalum wa kushiriki sensa ya watu na makazi ukiimbwa na kwaya ya Agape kutoka katika kikundi cha Upendo cha Wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wakati alipofika kuzungumza na wananchi wa Wilaya hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Dkt. Philip Mpango akicheza wimbo na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Inyonga iliopo  Wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wakati alipofika kuzungumza na wananchi wa Wilaya hiyo.

            

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Viongozi pamoja na wananchi wa Wilaya ya Mlele mkoani Katavi wakati wa ziara yake katika mkoa hu ol

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Dkt. Philip Mpango ameigiza Wizara ya Nishati kuhakikisha ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme wa Gridi ya Taifa cha Inyonga kukamilika ifikapo Oktoba mwaka 2023 na mkoa wa Katavi unaunganishwa katika Gridi ya Taifa.

Makamu wa Rais amesema alipokuwa akizungumza na viongozi na wananchi wa Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi  mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme wa  msongo wa Kilovoti 132 kutoka Tabora hadi Katavi katika eneo la Inyonga Wilaya ya Mlele. Makamu wa Rais ameonesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo ambao umechelewa kwa takribani miezi nane mpaka sasa.

Halikadhalika Makamu wa Rais amewataka wakurugenzi kuacha mara moja tabia ya kutoza ushuru kwa mazao yanayosafirishwa chini ya tani moja kwani serikali ilionmdoa tozo hizo ili kuwasaidia wakulima wadogo kupata kipato. Amesema wakurugenzi wanapaswa kutafuta mbinu sahihi za kuwabaini wanaokusanya mazao zaidi ya tani moja ili kuwanusuru wale wakulima wadogo.

Pia Makamu wa Rais amewaasa wananchi wa Mlele kuendelea kutafuta elimu kuhusu lishe ili wananchi wa mkoa huo wawe na afya bora kulingana na mazao mengi wanayozalisha. Makamu wa Rais amewataka kuendelea na juhudi za kutunza mazingira ikiwemo kupiga vita uchomaji miti na uchafuzi wa mazingira. 

Makamu wa Rais amewaagiza wazazi na walezi mkoa wa Katavi  kuhakikisha watoto wao wanapata elimu ili taifa kuwa na rasilimali bora zaidi itakayoharakisha maendeleo.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mheshimiwa Mwamvua Mrindoko ameishukuru Serikali kwa kuuwezesha mkoa huo kwa miradi mbalimbali inayochochea maendeleo kama vile miradi ya elimu, maji, barabara, afya pamoja kuongezewa idadi ya watumishi wapatao 692 katika sekta ya afya na elimu kwa mara moja.

Aidha Mkuu wa Mkoa amemueleza Makamu wa Rais maendeleo ya sekta ya kilimo mkoani Katavi iliopelekea kupatikana kwa mazao ya kutosha. Amesema jumla ya tani zaidi ya laki tisa za mazao ya chakula zimevunwa mwaka huu na kufanya ziada ya chakula kuwa tani  zaidi ya laki tano  katika mkoa huo. Amewaasa wazazi na walezi kuendelea kuweka akiba ya chakula pamoja na kuhakikisha biashara ya mazao inatumika kuhudumia watoto wao katika kupata elimu na mahitaji muhimu.

Awali akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Mlele, Mbunge wa Jimbo hilo Mheshimiwa Isaac Kamwele ameiomba serikali kukamilisha ujenzi wa majosho sita ili kuwasaidia wananchi wa eneo hilo ambao wengi wao ni wakulima na wafugaji. Pia ameongeza kwamba kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wananchi wananchi hao wanahitaji shule mbili zaidi za elimu ya msingi pamoja na Chuo cha Veta kitakachowasaidia katika kupata ujuzi.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango yupo ziarani mkoani Katavi ambapo anakagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.





Matangazo

  • TANGAZO KUTOKA TUME HURU YA UCHAGUZI March 03, 2025
  • MABADILIKO YA UKUMBI WA USAILI MLELE DC October 04, 2024
  • Tangazo la Ajira ya ukusanyaji wa Mapato July 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI MBALIMBALI ZA AFYA December 10, 2021
  • Waonaji wote

Habari Mpya

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE SHIKIZI

    April 03, 2025
  • KIKAO CHA WAMILIKI WA VIWANDA VYA KUCHAKATA UNGA

    March 14, 2025
  • MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA TEA KUKABIDHI MIRADI

    February 22, 2025
  • MSAADA WA MADAWATI 136

    January 30, 2025
  • Waonaji wote

Video

#TBC LIVE ZOOM: YALIYOJIRI NA MAFANIKIO YA ZIARA YA RAIS SAMIA NCHINI QATAR
Video Zaidi

wavuti za Haraka

  • FACE BOOK PAGE YA MLELE
  • MLELE DC BLOG
  • kilimo na umwagiliaji
  • mafunzo tovuti za serikali kanda ya magharibi
  • MAONESHO
  • Tuma barua pepe hapa

Wavuti Mwambata

  • Wizara ya Utumishi wa Umma
  • Tume ya ajira ya Tanzania
  • Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania
  • Jamhuri ya muungano wa tanzania
  • Tawala za mikoa na Serikali za mitaa
  • BARAZA LA MITIHANI

Takwimu za Watembeleaji

world map hits counter

Hesabu Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele

    Anuani ya Posta: S.L.P 686 MPANDA

    Simu: +25525295197

    Simu ya Kiganjani: 0786077372

    Barua pepe: ded@mleledc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ya @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Hakizote zimehifadhiwa