Halmashauri yatoa Mkopo kwa Vikundi vya Wajasiliamali wanawake ,Vijana na watu wenye ulemavu.
Halmashauri ya wilaya ya Mlele imeendelea kutekeleza lengo la kuboresha hali ya maisha ya wananchi kijamii na kiuchumi kwa kutoa mikopo ya kwa vikundi 14 kwa wanawake Vijana na watu wenye ulemavu, kwa kipindi cha julai hadi Novemba mwaka kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2020/2021 mkopo huu ni kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kuhakikisha asilimia ya kumi ya mapato ya ndani yanayotengwa kwa ajili ya kuwawezesha wajasiliamali,wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu kutekeleza shughuli zao za ujasiliamali wenye tija.
Akizungumzia utoaji wa mikopo hiyo kwa vikundi vya Wajasiliamali wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadiili mpango na Bajeti uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari Inyonga Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mwl Alexius Revocatus Kagunze ameeleza kuwa Halmashauri ya Mlele jumla ya shilingi milioni 60 zimekopeshwa kwa jumla ya vikundi,ikiwa ni vikundi 14 vya wanawake vinane, Vijana vikundi vitano na watu wenye ulemavu kikundi kimoja.
Kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri ya Wilaya ililenga kutoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya wanawake milioni Vijana milioni na watu wenye ulemavu milioni yenye thamani ya shilingi 72 milioni hadi kufikia Novemba 2021 Halmashuri imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi 62.5 milioni, ambapo wanawake walipata milioni 31,Vijana 26.5 milioni na watu wenye ulemavu walipata milioni tano.
Mkurugenzi huyo amesema manufa yanayotarajiwa baada ya kutoa mikopo hii ni pamoja na kurejesha vikundi kupanua mtaji,kuongeza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zitakazokidhi mahitaji ya soko na kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa walengwa.
Manufaa mengine ni kuchochea utengenezaji na upatikanaji wa ajira kwa vijana kuwaepusha wanufaika na vitendo hatarishi vinavyochochea mmomonyoko wa maadili na uvunjifu wa amani.
Ukuaji wa Uchumi wa kaya na jamii na kupunguza umasikini,pia Halmashauri itaongeza mapato kupitia vyanzo vyake vinavyoelekeana na shughuli za wajasiliana.
Mwisho.
Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
Anuani ya Posta: S.L.P 686 MPANDA
Simu: +255759023788
Simu ya Kiganjani: 0759023788
Barua pepe: ded@mleledc.go.tz
Hakimiliki ya @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Hakizote zimehifadhiwa