TAARIFA YA UTEKELEZAJI - IDARA YA MAJI KWA KIPINDI CHA MWEZI JULAI HADI DISEMBA KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017
UTANGULIZI
Idara ya maji ni miongoni mwa Idara zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Katika kutekeleza shughuli zake, imegawanyika katika vitengo vifuatavyo:-
Halmashauri ilikuwa na jumla ya wananchi 34,960 kwa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, kwa mwaka 2016 Halmashauri yetu inakadiriwa kuwa na wananchi 39,654 ikiwa ni wastani wa ongezeko la watu kwa asilimia 3.2 kila mwaka. Mpaka sasa ni asilimia 42.1 ya wananchi ndio wanaopata huduma ya maji safi na salama.
Watumishi wa Idara
Idara hii ina jumla ya watumishi 5 katika mchanganuo ufuatao:-
Fundi sanifu - maji (2, Mmoja kujitolea)
HALI YA USAMBAZAJI HUDUMA YA MAJI
Hali ya usambazaji wa huduma ya Maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele inategemea uwepo wa miundo ifuatayo:-
Visima virefu
Halmashauri ya wilaya ya Mlele ina visima virefu 134 ambavyo vinatumia pampu ya mkono katika kutoa huduma ya maji kwa wananchi.
Visima vifupi
Halmashauri ya wilaya ya Mlele haina visima vifupi
Miradi ya maji ya kusukuma kwa mashine inayotumia dizeli
Katika kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wananchi Halmashauri ya Wilaya ya Mlele itatekeleza ujenzi wa miradi ya kusukuma kwa mashine inayotumia dizeli/umeme jua kwa ajili ya kuwapatia wananchi huduma ya maji.
Miradi ya maji safi na usafi wa mazingira itakayotekelezwa ni miradi ya maji katika vijiji vya Nsenkwa, Mapili, Ilunde, Wachawaseme, Inyonga na Kamsisi.
Miradi tajwa hapo juu ipo hatua ya zabuni na utekelezaji wake utaanza Januari, 2017.
Miradi iliyokamilika ni ukarabati wa visima, uchimbaji wa visima ishirini na moja katika vijiji vya Kamsisi, Songambele, Imalauduki, Inyonga, Kalovya, Kamalampaka, Mapili, Ipwaga, Mlogoro, Kaulolo, Nsenkwa, Mtakuja, Wachawaseme, Utende, Ilunde na Isegenezya na tayari visima vyote ishirini na moja vinatumika kama ilivyokusudiwa.
Mifumo ya uvunaji maji ya mvua
Halmashauri pia itatekeleza ujenzi wa miradi ya uvunaji maji ya mvua katika baadhi ya maeneo ili kuondoa tatizo la maji kwa wananchi. Mfano wa miradi hiyo ni miradi ya uvunaji maji ya mvua Inyonga, Ilunde na Wachawaseme. Pia wananchi wamekuwa wakihamasishwa kutekeleza mifumo ya uvunaji wa maji ya mvua katika kukabiliana na tatizo la maji kwa wananchi wetu.
Maji ya kutega
Pia katika kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa uhakika kwa wananchi Halmashauri ipo katika hatua ya usanifu wa ujenzi wa Mabwawa mawili katika Kata ya Nsenkwa na Ilunde, maamuzi ya usanifu yaliamuliwa na timu maalumu iliyotumwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kubaini maeneo yenye sifa za kujengwa Bwawa, Timu hii ilifanya utafiti na kubaini maeneo tajwa hapo juu yanasifa.
MALENGO YA IDARA YA MAJI:
HALI YA UTEKELEZAJI WA MALENGO YA IDARA
Halmashauri kupitia Idara ya Maji katika kuhakikisha inatimiza wajibu wake wa kupeleka huduma ya maji kwa wananchi na kutekeleza malengo ya kiidara imesimamia na kutekeleza yafuatayo:-
Usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maji iliyokamilika ambapo huduma ya maji inapatikana kwa uhakika.
NA. |
KIJIJI
|
AINA YA MRADI |
MAELEZO
mmmmm/MMMMMMMMmmm |
1.
|
Mapili
|
Uchimbaji wa visima viwili virefu
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa.
|
2.
|
Ipwaga
|
Uchimbaji wa kisima kirefu
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa.
|
3
|
Mtakuja
|
Uchimbaji wa kisima kirefu
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa.
|
4.
|
Kaulolo
|
Uchimbaji wa kisima kirefu
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa.
|
5
|
Nsenkwa
|
Uchimbaji wa kisima kirefu
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa.
|
6
|
Wachawaseme
|
Uchimbaji wa kisima kirefu
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa..
|
7
|
Utende
|
Uchimbaji wa kisima kirefu
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa.
|
8
|
Inyonga
|
Uchimbaji wa kisima kirefu
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa.
|
9
|
Kamalampaka
|
Uchimbaji wa visima viwili virefu.
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa.
|
10
|
Kalovya
|
Uchimbaji wa visima viwili virefu
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa.
|
11
|
Kamsisi
|
Uchimbaji wa visima viwili virefu
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa..
|
12
|
Songambele
|
Uchimbaji wa kisima kirefu
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa.
|
13
|
Imalauduki
|
Uchimbaji wa kisima kirefu
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa.
|
14
|
Nsenkwa
|
Uchimbaji wa kisima kirefu
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa..
|
15
|
Ilunde
|
Uchimbaji wa kisima kirefu
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa.
|
16
|
Isegenezya
|
Uchimbaji wa Visima viwili virefu
|
Kazi ya uchimbaji imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa.
|
Usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maji inayotekelezwa chini ya mpango wa maendeleo ya sekta ya maji kwa ufadhili wa wahisani na Serikali ya Jamhuri ya Tanzania
NA
|
KIJIJI
|
AINA YA MRADI ILIYOTEKELEZWA
|
HATUA YA UTEKELEZAJI
|
MAELEZO
|
1.
|
Mamba
|
Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Mamba unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania.
|
Utekelezaji wa mradi huu umekamilika na mradi unatumika pia mradi upo hatua ya matazamio.
|
Utekelezaji wa mradi huu umekamilika na mradi unatumika pia mradi upo hatua ya matazamio.
|
Ujenzi wa miradi mipya
NA
|
KIJIJI
|
AINA YA MRADI
|
HATUA YA UTEKELEZAJI
mmmmm/MMMMMMMMmmm |
GHARAMA/MAELEZO
|
1
|
Mapili
|
Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Mapili unaofadhiliwa na Serikali ya Tanzania.
|
Utekelezaji wa mradi huu upo hatua ya Zabuni.
|
Utekelezaji wa mradi huu upo hatua ya zabuni.
|
2
|
Nsenkwa
|
Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Nsenkwa unaofadhiliwa na Serikali ya Tanzania.
|
Utekelezaji wa mradi huu upo hatua ya Zabuni.
|
Utekelezaji wa mradi huu upo hatua ya zabuni.
|
3
|
Inyonga
|
Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Inyonga unaofadhiliwa na Serikali ya Tanzania.
|
Utekelezaji wa mradi huu upo hatua ya Zabuni.
|
Utekelezaji wa mradi huu upo hatua ya zabuni.
|
4
|
Wachawaseme
|
Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Wachawaseme unaofadhiliwa na Serikali ya Tanzania.
|
Utekelezaji wa mradi huu upo hatua ya Zabuni.
|
Utekelezaji wa mradi huu upo hatua ya zabuni.
|
5
|
Ilunde
|
Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Ilunde unaofadhiliwa na Serikali ya Tanzania.
|
Utekelezaji wa mradi huu upo hatua ya Zabuni.
|
Utekelezaji wa mradi huu upo hatua ya zabuni.
|
6
|
Kamsisi
|
Mradi wa maji ya bomba katika kijiji cha Kamsisi unaofadhiliwa na Serikali ya Tanzania.
|
Utekelezaji wa mradi huu upo hatua ya Zabuni.
|
Utekelezaji wa mradi huu upo hatua ya zabuni.
|
Kutoa elimu ya usafi wa mazingira na uundwaji wa jumuiya za watumiaji maji.
Katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2016/2017 palikuwa na zoezi la utoaji wa mafunzo kwa jumuiya za watumiaji maji na usajili wa jumuiya za watumiaji maji.
Elimu ya usafi wa mazingira na unawaji mikono kabla ya kula, unawaji mikono kwa maji na sabuni baada ya kutoka chooni elimu hii huletwa kupitia programu ya SWASH na programu ya usambazaji maji vijijini (RWSSP) chini ya kipengele cha usafi wa mazingira. Utekelezaji wa elimu hii utasaidia kupunguza magonjwa ya mlipuko kwa wananchi hasa watoto. Hakukuwa na utoaji wa huduma hii kutokana na tatizo la ukosefu wa fedha.
Uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji
Elimu ya utunzaji / uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji ilitolewa wakati wa zoezi la usajili wa jumuiya za watumiaji maji (COWSOs) kutokana na ukosefu wa fedha za utekelezaji.
CHANGAMOTO:
Halmashauri kupitia idara ya maji inakabiliwa na changamoto zifuatazo katika utekelezaji wa majukumu yake:-
UTATUZI WA CHANGAMOTO
Naomba kuwasilisha
Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
Anuani ya Posta: S.L.P 686 MPANDA
Simu: +255759023788
Simu ya Kiganjani: 0759023788
Barua pepe: ded@mleledc.go.tz
Hakimiliki ya @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Hakizote zimehifadhiwa