• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watuishi |
Mlele District Council
Mlele District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Msingi Mkuu
    • Mpango Mkakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Maji
        • Historia
        • Dhima na Dira
        • Muundo wa Taasisi
        • Ukaribisho
        • Huduma
        • Jaribu
        • what we do
        • Huduma ya Maji
        • Huduma za Afya
        • Elimu Msingi
        • Huduma
        • Mwenyekiti wa Halmashauri
        • Mkurugenzi Mtendaji
        • Utawala na Rasilimali watu
        • /TEHAMA-na-Takwimu
        • Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii
        • Mipango takwimu na Ufuatiaji
        • Ardhi na Maliasili
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Sheria
        • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Maendeleo ya Jamii
        • Idara
        • Vitengo
        • Ujenzi
        • Maji
        • Ugavi na Manunuzi
        • Usafishaji na Mazingira
        • Uchaguzi
        • Tasaf III
        • Mainstreaming Sustainable Forest Managment in Woodland of Western Tanzania Project
        • Mwenge waUhuru
        • UKIMWI/ VVU
        • Risk Oficer Cordinator
        • Miradi inayoendelea
        • Zabuni
        • Kazi za Idara Utumishi
        • Muundo wa Halmashauri
        • Miradi Lengwa
        • Kitengo cha nyuki
        • Mwenge
        • Sera ya Faragha
        • Kanusho
        • Machapisho
        • Sheria
        • MTF
        • Fomu
        • Orodha ya Madiwani
        • Fedha, Uongozi na Mipango
        • UKIMWI
        • Maji
        • Mipango Miji na Mazingira
        • Uchumi, Afya na Elimu
        • Maadili
        • Ratiba
        • Vikao vya waheshimiwa
        • Kuonana na Mwenyekiti
        • Madiwani
        • Kanausho
        • Huduma ya Maji
        • Huduma ya Afya
        • Huduma ya Kilimo
        • Huduma ya Elimu
        • Huduma ya Ufugaji
        • Huduma za Uvuvi
        • Huduma za Sheria
        • Huduma za kiutumishi
        • Vivutio vya Utalii
        • Kilimo
        • Ufugaji
        • Itakayo tekelezwa
        • Inayoendelea
        • Iliyo Tekelezwa
        • muongozo
        • Sheria Ndogo
        • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
        • Mpango Mkakati
        • Taarifa
        • Fomu Mbalimbali
        • Taarifa kwa Umma
        • Video za shughuli zetu
        • Maktaba ya Picha
        • Magazeti
        • Hotuba
        • ORODHA YA WAJUMBE WA KAMATI MBALIMBALI ZA KUDUMUKWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020
        • KARENDA YA VIKAO VYA KISHERIA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA MLELE KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya
    • Viengo
      • Kitengo cha TEHAMA na Mahusiano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Uchaguzi Uchaguzi
      • Kitengo cha nyuki
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Huduma za Kilimo
    • Uvuvi
    • Elimu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orotha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Mazingira
      • UKIMWI
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa
      • Kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Mkataba wa Huduma
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
  • Kiini cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Album ya Picha
    • Video
    • Hotuba
  • TASAF

miombo

Start Date: 2013-10-01
End Date: 2017-07-01

MRADI WA USIMAMIZI ENDELEVU WA MISITU YA MIOMBO MAGHARIBI MWA TANZANIA KATIKA WILAYA YA MLELE. 

UTANGULIZI

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Misitu ya Miombo  Magharibi mwa Tanzania ni mradi wa miaka mitano ulizinduliwa mwaka 2013. Mradi huu unatekelezwa katika Wilaya nne za Urambo, Uyui na Kaliua za Mkoa wa Tabora na Wilaya ya Mlele ya Mkoa wa Katavi. Katika wilaya ya Mlele mradi unatekelezwa katika vijiji tisa vya Inyonga, Kaulolo, Nsenkwa, Kamsisi, Mtakuja, Kalovya, Kamalampaka, Songambele na Imalauduki.

Mradi huu unafadhiliwa kwa pamoja na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF), Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Lengo kuu la Mradi huu ni kuwa na Usimamizi Endelevu wa Misitu ili kulinda mfumo wa Ikolojia na Bayoanuai na kuwa kinga kwa Misitu ya mvua ya Kongo, kuwa na usalama wa chakula na maisha bora kwa wananchi. 

Lengo mahususi la Mradi ni kuwezesha jamii zinazo ishi kandokando ya misitu kwa kutegemea misitu kuwa na njia mbadala za uzalishaji ambazo ni rafiki kwa mazingira na zitakazo boresha hali ya maisha ya jamii hizo.

Misitu ya Miombo inachukua sehemu kubwa ya eneo la wilaya ya mlele ina manufaa mbalimbali kwa jamii zinazoishi kandokando ya misitu hiyo na kwa taifa kwa ujumla, kwa kuwa ni chanzo cha Nishati kama Kuni na Mkaa, chanzo cha bidhaa muhimu kama Mijengeo, Nguzo, Mbao, Vyombo vya nyumbani, Chakula, Madawa na Malisho. Pia misitu hii hutoa huduma za kiiokolojia kama Makazi ya viumbe hai na kutunza hewa ukaa hivyo kurekebisha athari za mabadiliko ya tabia nchi, kuzuia mmomonyoko wa udongo, chanzo cha kivuli, kuboresha mzunguko wa haidrolojia na kutunza rutuba ya udongo.

Pamoja na kuwa na manufaa yote hayo, Misitu ya miombo imekuwa ikiharibiwa kwa kasi na shughuli mbalimbali za binadamu kama ukataji miti  hovyo, uvamizi wenye lengo la kuanzisha makazi ndani ya misitu, kilimo cha kuhama hama na uanzishwaji wa mashamba katika  maeneo ya misitu, uvunaji wa mbao na magogo, uvunaji wa kuni kwa ajili ya kukaushia tumbaku, uchomaji mkaa, mabadiliko ya tabia nchi n.k.

Suluhu ya muda mrefu kwa uharibifu wa misitu hii ni kutwaa desturi ya usimamizi na matumizi endelevu  na kudhibiti shughuli za kibiashara za rasilimali hizi kitu ambacho mradi huu unatekeleza.

Mradi huu unatekelezwa kupitia vipengele vikuu vinne ambavyo ni;

Urekebishaji wa sera na mpangilio wa taasisi kusaidia usimamizi endelevu wa misitu.

Kuimarisha ujuzi na uwezo wa maarifa kwa usimamizi wa misitu ya jamii/ usimamizi shirikishi wa misitu, usimamizi wa rutuba ya udongo na matumizi bora ya ardhi.

Uzalishaji endelevu wa mkaa na nishati mbadala ili kupunguza msukumo katika uvunaji wa misitu.

Kusaidia masoko na teknolojia kwa ajili ya kupunguza msukumo wa uharibifu katika kilimo na rasilimali asili na kuongeza kipato.

UTEKELEZAJI.

Kwa kipindi cha kuanzia octoba 2013 hadi juni  2016, Mradi wa miombo umefanikiwa kutekeleza yafuatayo katika wilaya ya mlele;

  1. KIPENGELE CHA UREKEBISHAJI WA SERA, SHERIA NA MPANGILIO WA TAASISI KUSAIDIA USIMAMIZI ENDELEVU WA MISITU.

 MAPITIO YA SERA ZA KISEKTA

Wataalam  kutoka sekta za misitu, mifugo, kilimo, na ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlele walishiriki  katika kufanya mapitio ya sera mbalimbali zinazohusiana na usimamizi wa misitu kazi iliyoongozwa  na mtaalam elekezi aliyepewa kazi na mradi ya kufanya mapitio kwa lengo la kutambua migongano, ombwe na muingiliano kati ya sera za sekta hizo katika kutoa muongozo wa usimamizi endelevu wa misitu kisha kuzifanyia marekebisho yatakayo wezesha kuwa na sera zitakazopelekea  ufanisi katika usimamizi endelevu wa misitu

  MAPITIO YA SHERIA NDOGO ZA VIJIJI

Kwa kutumia washauri elekezi na wataalam wa halmashauri, mradi ulifanya mapitio ya sheria ndogo za vijiji katika vijiji vya Kamsisi na Nsenkwa ili kuona ufanisi wake katika usimamizi endelevu wa misitu. Baada ya kazi hii, kijiji cha Kamsisi kimetunga  sheria ndogo za kijiji hicho ambazo zina ufanisi zaidi katika kusimamia misitu.

  1. KIPENGELE CHA KUIMARISHA UJUZI NA UWEZO WA MAARIFA KWA USIMAMIZI WA MISITU YA JAMII/ USIMAMIZI SHIRIKISHI WA MISITU, USIMAMIZI WA RUTUBA YA UDONGO NA MATUMIZI BORA YA ARDHI.

2.1 MAFUNZO

Katika kuimarisha ujuzi na uwezo wa maarifa kwa usimamizi wa misitu ya jamii au/na usimamizi shirikishi wa misitu, usimamizi wa rutuba ya udongo na matumizi bora ya ardhi. Mradi umewezesha mafunzo mbalimbali kwa wakulima,wajumbe wa serikali ya kijiji na  kamati za maliasili na mazingira za vijiji, wataalam wa halimashauri na wadau wengine kama ilivyo orodheshwa katika jedwali hapo chini.

NA
AINA YA MAFUNZO
WASHIRIKI
IDADI YA WASHIRIKI
JINSI
KE
ME
1
Umuhimu wa kuzingatia  jinsia katika utunzaji wa misitu
Wataalam halmashauri, kata na vijiji
23
2
21
2
Dhana na utekelezaji wa  shamba darasa
Wataalam halmashauri, kata na vijiji
23
2
21
3
Ufugaji bora wa nyuki
Vikundi vya wafugaji nyuki katika vijiji vya mradi
236
58
178
4
Kilimo bora cha bustani kwa kufuata kanuni zitakazo punguza athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa mkulima
Wakulima wa bustani kutoka vijiji vya mradi
55
17
38
5
Kilimo Hifadhi
Maafisa ughani na wakulima wa kijiji cha Kamsisi
15
8
7
6
Usimamizi wa rutuba ya udongo
Maafisa ughani na wakulima
15
2
13
7
Utunzaji wa mazingira
Kamati ya maliasili na mazingira za vijiji
72
24
48
8
Uanzishaji na utunzaji wa bustani za miti
Wakulima wa bustani za miti
15
0
15
9
Uandaaji wa mipango ya maendeleo ngazi za mkoa, wilaya, kata na kijiji
Wataalam wa wilaya , kata na vijijini.na  Viongozi wa serikali za vijiji
16
2
14
10
Mafunzo ya ujasiliamali
Wajasiliamali
80
46
34
11
Ushonaji mavazi ya kuvunia asali
Mafundi cherehani kutoka vijiji vya 5 vya mradi
10
4
6
12
Kilimo bora cha uyoga
Wakulima kutoka kijiji cha kamalampaka na Mtakuja
12
4
8
13
Mafunzo ya ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu na taarifa za hali ya misitu.
Wataalam wa halmashauri na mwakilishi wa kamati ya maliasili ya kijiji cha Kamsisi
4
0
4

 

 SHAMBA DARASA

Mradi wa miombo una lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao makuu katika vijiji vya mradi kwa angalau asilimia 25 ili kuongeza usalama wa chakula katika vijiji hivyo. Ili kufikia lengo hilo mradi wa miombo umewezesha utekelezaji wa mashamba darasa na mashamba ya mfano ya mazao ya Mahindi, Alzeti na Karanga katika vijiji vya mradi kwa misimu ya mwaka 2013/2014 na  2014/2015  yakiwa na lengo la kuonesha au/na kusambaza mbinu  bora za kilimo.

Jedwali hapa chini linaonesha uzalishaji katika mashamba darasa na mfano hayo  ikilinganishwa na uzalishaji wa kawaida wa wakulima wengi wa vijiji hivyo.

NA
MSIMU
AINA YA ZAO
WASHIRIKI
MAVUNO SHAMBA DARASA /EKARI
MAVUNO KILIMO CHA KIENYEJI /EKARI
1
2013/2014
Mahindi
Wakulima 122 wa vijiji 5 vya awali vya mradi
Gunia 20 za kilo 90
Gunia 7 za kilo 90
2
2014/2015
Alzeti
Wakulima 15
Wastani wa gunia 15 za kilo 60
Wastani wa gunia 3 za kilo 60

. KAMATI ZA MALIASILI NA MAZINGIRA ZA VIJIJI.

Ili kuwezesha usimamizi wa misitu katika vijiji kuwa endelevu, Mradi umewezesha uuandwaji wa kamati za maliasili na mazingira za vijiji katika vijiji sita vya Kamsisi, Inyonga, Nsenkwa, Kaulolo, Mtakuja na Kamalampaka. Kamati hii ni kamati ndogo ya kijiji chini ya Kamati ya huduma za jamii ya kijiji na ipo chini ya serikali ya kijiji. Kamati hii ina wajumbe 12 ambao theluthi ya wajumbe ni wanawake na wajumbe hao huteuliwa na serikali ya kijiji na kupitishwa na mkutano mkuu wa kijiji. Kamati hii imepatiwa mafunzo ya utunzaji wa misitu na wajibu wao katika utunzaji wa misitu inayowazunguka na ina jukumu la kusimamia shughuli zote za usimamizi/utunzani mazingira katika kijiji.

. UTENGENEZAJI MAJIKO BANIFU YA KUPIKIA.

Majiko banifu ni aina ya majiko ya kupikia ambayo hutumia kuni chache ikilinganisha na majiko ya kawaida ya mafiga matatu. Ili kupunguza matumizi ya kuni katika kupikia mradi umewezesha utengenezwaji majiko banifu katika vijiji vya mradi, hii ni baada ya kutoa mafunzo ya ujenzi wa majiko hayo kwa vikundi vya wanawake kutoka vijiji 7 vya mradi. Mafundi hao wamejenga majiko banifu 412 katika vijiji hivyo. Uzoefu umeonesha majiko haya yanaweza kupunguza matumizi ya kiasi kikubwa cha kuni. Mfano kwa tathimini iliyofanyika katika kijiji cha Kamsisi kwa Mama Fortunate John ambaye alikuwa akitumia kuni kiasi cha mzigo moja wa kwa siku tatu kwa kutumia majiko ya kawaida sasa anatumia mzigo moja kupikia kwa kipindi cha wiki mbili kwa kutumia jiko banifu.

      2.5  UWEKAJI WA MIPAKA YA KUDUMU NA KUFANYA TATHMINI YA MSITU.

Mradi umewezesha upimaji na uwekaji wa mipaka ya kudumu katika msitu wa kijiji cha Kamsisi wenye ukubwa wa hekta 199. Mawe ya mpakani (Beacon) 20 yamejengwa na kupakwa rangi katika mipaka ya msitu huo. Pia mradi umefanya tathmini ya msitu kutambua rasilimali zilizopo katika msitu

2.7 UCHUNGUZI WA HALI YA RUTUBA YA UDONGO

Mradi umewezesha uchunguzi wa rutuba ya udongo katika vijiji vya Nsenkwa na kamsisi ambao ulikuwa na lengo la kuchunguza hali ya rutuba ya udongo na kutumia matokeo ya uchunguzi kushauri wakulima juu ya mbinu bora za kusimamia rutuba ya udongo huo ili kuongeza uzalishaji na kupunguza uharibifu wa ardhi na misitu unaosababishwa na kilimo cha kuhamahama kutafuta maeneo yenye rutuba. Mkutano wa hamasa umefanyika katika kijiji cha Kamsisi ambapo wananchi walielimishwa juu ya  hali ya rutuba na afya ya udongo wa eneo hilo na  ushauri wa namna ya kuboresha na kusimamia rutuba ya udongo ulitolewa. Matumizi sahihi ya ushauri unaotolewa kutokana na matokeo ya uchunguzi huo yatawezaongeza uzalishaji wa kilimo na kupunguza mahitaji ya mashamba mapya hivyo kulinda misitu dhidi ya uharibifu unaosababishwa na kilimo cha kuhama hama na ufunguzi wa mashamba ndani ya misitu.

2.8  UTAFITI KWA VITENDO SHIRIKISHI WA ZAO LA MAHINDI.

Mradi umetekeleza utafiti kwa vitendo shirikishi wa kilimo cha zao la mahindi katika kijiji cha Kamsisi juu ya usimamizi wa rutuba ya udongo katika msimu wa 2014/2015. Utafiti kwa vitendo shirikishi ni aina ya utafiti ambao hufanywa kwa pamoja kati ya watafiti, maafisa ughani na wakulima shambani kwa mkulima. Utafiti huu ulikuwa ukipima uzalishaji wa mahindi kwa kutumia aina tofauti za mbolea kwa kufuata kanuni za kilimo hifadhi. Utafiti huu ulitekelezwa na wakulima 9 na Kulikua na vishamba vinne vya majaribio kwa kila mkulima. Vishamba hivyo vilikua ni , kishamba kiongozi kilicholimwa kwa mazoea ya mkulima, kishamba kilicho pandiwa mbolea ya minjingu mazao na kukuzia mbolea ya urea, kishamba kilichopandiwa mbolea ya yaramila cereal na kukuzia yarabela sulfan, kishamba kilichopandiwa mbolea ya  samadi na kukuzia mbolea ya yarabela sulfani. Matokeo ya utafiti huu ni kama inavyoonekana katika jedwali hapo chini;

NA
AINA YA KISHAMBA
MAVUNO (Tan/Ha)
1
Kiongozi
0.33
2
Minjingu mazao +urea
3.2
3
Yaramila cereal + yarabela sulfan
5.6
4
Samadi + yarabela sulfan
3.6




3.0 KIPENGELE CHA UZALISHAJI ENDELEVU WA MKAA NA NISHATI MBADALA ILI KUPUNGUZA  UVUNAJI WA MISITU.

Katika kipengele hiki mradi umetekeleza yafuatayo;

3.1 UWEZESHAJI WA MASHINE YA KUTENGENEZEA MKAA.

Katika kusaidia teknolojia ambayo itapunguza uharibifu wa misitu kwa uchomaji mkaa, Mradi umewawezesha wajasiliamali wenye mashine za kuchana mbao wa mpanda na inyonga kwa kuwapatia mashine za kutengenezea mkaa kutokana na mabaki ya mbao na mazao kwa makubaliano maalum ya kuzalisha mkaa na kuutafutia soko. Mkaa utakao tengenezwa na mashine hizi utakua mbadala wa mkaa unao zalishwa kwa kukata miti hivyo kupunguza mahitaji ya mkaa wa miti na uharibifu wa misitu. Pia mradi umeviwezesha vikundi vya wanawake vya Nsenkwa na Inyonga kwa kuwapatia mashine ndogo za kuzalisha mkaa 5 za kawaida na 2 za umeme baada ya kuwapa mafunzo ya utengenezaji wa mkaa huo. Vikundi hivi vimeshaanza uzalishaji na uzalishaji unategemewa kuongezeka kama soko litaongezeka.

3.2. UJENZI WA MFUMO WA BIOLATRINE SHULE YA SEKONDARI INYONGA.

Ili kupunguza matumizi ya kuni katika kupikia, Mradi wa miombo umetekeleza ujenzi wa mfumo wa bayolatrine katika shule ya sekondari ya inyonga ambao utatumia kinyesi cha binadamu kuzalisha gesi aina ya methane ambayo itatumika kama chanzo cha nishati katika kupikia, mwanga na mbolea kwa ajili ya bustani.  Hii itapelekea kupunguza matumizi ya kuni na mkaa katika taasisi hiyo hivyo kupunguza uhalibifu wa misitu.

3.3. ZIARA YA MAFUNZO YA UCHOMAJI WA TUMBAKU KWA KUTUMIA MABANI BANIFU.

Mradi umewezesha ziara ya mafunzo ya uchomaji wa tumbaku kwa kutumia majiko banifu kwa wakulima 10, viongozi wa chama  cha wakulima wa Tumbaku (Ukonongo) na wataalam wa halmashauri katika shamba la mbegu la tumbaku lililopo wilayani Urambo mkoani Tabora. Ziara hii ilikuwa na lengo la kuhamasisha na kuongeza uelewa wa wataalam na wakulima juu ya teknolojia mbalimbali za ukaushaji tumbaku ambazo hutumia kuni chache na zenye ujazo mdogo ambayo sehemu ya mti (matawi) badala ya mti mzima huvunwa kwa ajili ya kukaushia tumbaku. Matumizi ya teknolojia hizi yanaweza kupunguza uhalibifu wa misitu kwa kiwango kikubwa.

4.0 KIPENGERE CHA KUSAIDIA MASOKO NA TEKNOLOJIA KWA AJILI YA KUPUNGUZA MSUKUMO WA UHARIBIFU KATIKA KILIMO NA RASILIMALI ASILI NA KUONGEZA KIPATO.

Mradi umetekeleza shughuli mbalimbali za kusaidia masoko na teknolojia kwa ajili ya kupunguza msukumo wa uharibifu katika rasilimali asili na kuongeza kipato kama ifuatavyo

 UWEZESHAJI WA VIKUNDI VYA WAFUGAJI NYUKI

Ufugaji nyuki ni moja kati ya shughuli inayopewa kipaumbele katika mradi wa miombo ikiwa na lengo la kuziwezesha jamii zinazoishi kandokando ya misitu kwa kutegemea misitu kuwa chanzo cha mapato ambacho ni rafiki kwa misitu hivyo kupunguza shughuli za uharibifu zinazofanywa kwa lengo la kujiongezea kipato kama uchomaji Mkaa, upasuaji wa Mbao nk. Baada ya kutoa mafunzo ya ufugaji bora wa nyuki kwa wafugaji nyuki katika vijiji vya mradi, wafugaji nyuki walihamasika na kuunda vikundi vya wafugaji nyuki 15 katika vijiji 5 vya awali vinavyotekeleza mradi. Vikundi hivyo vilipewa Mizinga ya kisasa 590 (mizinga 35 kwa kila kikundi) yenye thamani ya Tshs 38,350,000/= kutoka taasisi zisizo za kiserikali za UDESO na ACT-RUKWA ambazo ziliwezeshwa na mradi wa miombo kiasi cha Tsh  91,000,000 kwa ajili ya kuziwezesha jamii zanazoishi kandokando za misitu. Fedha hizi pia zilitumika kununua vifaa vingine ka na mavazi ya kinga 45, mashine ya kukamulia asali 7, vifaa vya kupimia ubora wa asali 7, machujio 24 na vipurizio vya moshi 34 ambavyo viligawiwa kwa vikundi vya wafugaji nyuki.

UWEZESHAJI UFUGAJI WA SAMAKI KATIKA KIJIJI CHA KAMSISI.

Katika kufikia lengo la kuongeza kipato kwa wananchi kupitia njia mbadala za uzalishaji ambazo ni rafiki kwa mazingira, mradi umewezesha ufugaji wa samaki katika kijiji cha Kamsisi. Baada ya mradi kutoa mafunzo juu ya ufugaji wa samaki katika kijiji cha Kamsisi, wananchi wa kamsisi walihamasika na kuunda kikundi cha ufugaji wa samaki chenye wanachama 25 ambapo mradi uliwezesha uchimbaji wa bwawa na vifaranga 1000 vya samaki na chakula cha kuanzia kilo 100.  Uvunaji umeshafanyika na sasa uhamasishaji unafanyika ili kupata wafugaji binafsi kutoka ndani ya kijiji cha Kamsisi na nje ya kijiji hususani kwa vijiji vya mradi.

 UFUGAJI KUKU.

Mradi wa miombo umewezesha ufugaji bora wa kuku kwa vikundi viwili  kutoka vijiji vya Kamsisi na Nsenkwa ambapo vikundi vimechangia ujenzi wa mabanda na mitetea na mradi umechangia majogoo ya kisasa , bati za kuezekea mabanda na chakula cha kuanzia cha kuku. Pia mradi umesaidia mashine ya kutotoreshea vifaranga kwa kikundi cha ufugaji kuku cha Nsenkwa.

.  VIKUNDI VYA KUWEKA AKIBA NA KUKOPA.

Mradi wa miombo umetoa mafunzo ya kuweka akiba na kukopeshana akiba hizo miongoni mwa wanakikundi ili kuwezes ha upatikanaji wa mitaji midogo katika vijiji hivyo. Mafunzo hayo yalitolewa katika vikundi vinne ambavyo mpaka sasa vikundi viwili vinaendelea vizuri na vimeweza kuweka akiba ya kiasi cha 3,500,000/= na 1,900,000/= kwa kikundi cha Mapambano na Nyatusanga vya kamsisi kila kimoja ambapo hukopeshana akiba hizo kwa riba nafuu tofauti na kutumia mikopo hiyo kama mitaji kwa ajili ya kuwekeza katika miradi midogomidogo.

. KILIMO CHA UYOGA

Mradi wa miombo umetoa mafunzo ya kilimo bora cha uyoga kwa vijiji vya kamalampaka na Mtakuja kwa wakulima 12 (wanaume 8 na wanawake 4). Na baadae kuwezesha vikundi kwa kuwapatia vifaa vya ujenzi wa mabanda. Vikundi hivi vipo katika hatua za utekelezaji ambapo kamalampaka walishapanda na Mtakuja wapo katika maandalizi ya kupanda.

 ZIARA ZA MAFUNZO KWA WAKULIMA NA WAJASILIMALI

Mradi umewezesha ziara ya mafunzo kwa wakulima na wajasiamali 5 mkoani Kilimanjaro ambapo Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Ardhi (SLM) ambao ni mradi dada wa mradi huu ulitekelezwa. Huko wakulima na wajasilimali hao walijifunza kutoka kwa wakulima na wajasilimali wenzao wa Kilimanjaro walinufaika na mradi SLM walioafaulu na wale walioshindwa kufanikiwa,  kwa kutembelea miradi na kufanya majadiliano ambayo yatawawezesha kuiga kwa wale waliofanikiwa na kukwepa sababu  zilizo sababisha walioshindwa kushindwa.

 UTAFITI KUBAINISHA MASOKO  MAZAO SI TIMBAO NA BIDHAA ZAKE KUTOKA KATIKA MISITU YA MIOMBO

Katika kusaidia masoko kwa mazao yasiyo timbau ya misitu ya miombo yanayopatikana  vijijini , mradi ulifanya utafiti wa kubainisha masoko ya kawaida na maalum kwa mazao si timbao na bidhaa zake kutoka misitu ya miombo. Katika wilaya ya Mlele utafiti huu ulifanyika katika  kata za Nsenkwa na Kamsisi. Pamoja na mambo mengine taarifa ya  utafiti huu ulitoa mapendekezo yafuatayo;

Mradi unatakiwa ufuate na kutekeleza mfumo mkakati wa masoko utakaozingatia ukuaji wa biashara ya mazao si timbao na mnyororo wake wa thamani. Mfumo mkakati huu utaunganisha masoko yaliyopo na wazalishaji wa bidhaa kipaumbele za mazao si timbao  ili kuongeza thamani kwa kuchagua masoko sahihi, kuongeza faida kupitia masoko mbalimbali na kuendeleza biashara kiundelevu kwa kutafuta wateja na kuhakikisha yanahifadhiwa wakati wote

Mradi ujengee uwezo jamii na hasa vikundi vya ujasiriamali kwa mazao si timbao katika dhana ya uzalishaji endelevu kupitia uoteshaji mazao nje ya misitu ya miombo, teknolojia za usindikaji, uongezaji thamani, mbinu bora za kuhifadhi mazao na vifaa vyake. Vikundi hivi vita kuwa kama chachu au shamba darasa kwa wasiohamasika na baadae kuingia katika utekelezaji

Mradi usaidie uanzishwaji wa Mtandao wa wazalishaji mazao si timbao yenye tija kibiashara kwa kuunganisha vikundi na wazalishaji binafsi waliopo. 

Mradi umeshaanza kutekeleza mapendekezo haya mfano kuwajengea uwezo vikundi vya ujasiliamali kuotesha mazao si timbao nje ya msitu  kwa kutoa mafunzo na kuwezesha kilimo cha uyoga kama ilivyoelezewa hapo juu.

 KUWEZESHA WAJASILIMALI KUSHIRIKI MAONESHO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.

Mradi umewawezesha wajasiliamali wa mazao sio timbao kutoka vijiji vya mradi kushiriki maonesho ya kitaifa na kimataifa kama maonesho ya kimataifa ya saba saba ya Dar es salaam na maonesho ya nanenane kanda ya nyanda za juu kusini ya mbeya ikiwa kuwapa fursa wajasiliamali hawa kujitangaza na kutafuta masoko ya bidhaa zao

HITIMISHO

Kwa kipindi cha  miaka miwili na miezi saba mradi umewezesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika vijiji vya mradi ukiwa na lengo la kuziwezesha jamii zinazoishi kwa kutegemea misitu kuwa na njia mbadala za uzalishaji ambazo ni rafiki kwa mazingira na zitakazo boresha hali ya maisha ya jamii hizo wakati huo huo ukiwezesha kuwapo na Usimamizi Endelevu wa Misitu ili kulinda mfumo wa Ikolojia na Bayoanuai na kuifanya misitu hiyo kuwa kinga kwa Misitu ya mvua ya kongo, kuwa na usalama wa chakula na maisha bora kwa wananchi. Kwa kipindi hiki kifupi kuna mafanikio yamepatikana katika maeneo ya  kilimo, kupunguza matumizi ya nishati ya kuni na kuna maeneo mengine ambayo bado kuna changamoto kama kupunguza matumizi ya mabani ya kienyeji, uvamizi katika misitu ya vijiji na utekelezwaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi juhudi zaidi zimeelekezwa ili kuweza kufikiwa kwa malengo ya mradi.

Naomba kuwasilisha.

 

 

 

.

Matangazo

  • Matokeo ya darasa saba mtihani wa TAIFA December 01, 2022
  • Tangazo la Ajira ya ukusanyaji wa Mapato July 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI MBALIMBALI ZA AFYA December 10, 2021
  • Tangazo la kuitwa KAZINI December 23, 2021
  • Waonaji wote

Habari Mpya

  • ujenzi wa vyumba vya madarasa wakamilika.

    January 02, 2023
  • ujenzi wa vyumba vya madarasa wakamilika.

    January 02, 2023
  • ujenzi wa vyumba vya madarasa wakamilika.

    January 02, 2023
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MLELE YAPONGEZWA UKUSANYAJI MAPATO.

    December 15, 2022
  • Waonaji wote

Video

#TBC LIVE ZOOM: YALIYOJIRI NA MAFANIKIO YA ZIARA YA RAIS SAMIA NCHINI QATAR
Video Zaidi

wavuti za Haraka

  • FACE BOOK PAGE YA MLELE
  • MLELE DC BLOG
  • kilimo na umwagiliaji
  • mafunzo tovuti za serikali kanda ya magharibi
  • MAONESHO
  • Tuma barua pepe hapa

Wavuti Mwambata

  • Wizara ya Utumishi wa Umma
  • Tume ya ajira ya Tanzania
  • Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania
  • Jamhuri ya muungano wa tanzania
  • Tawala za mikoa na Serikali za mitaa
  • BARAZA LA MITIHANI

Takwimu za Watembeleaji

world map hits counter

Hesabu Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele

    Anuani ya Posta: S.L.P 686 MPANDA

    Simu: +25525295197

    Simu ya Kiganjani: 0762362950

    Barua pepe: ded@mleledc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ya @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Hakizote zimehifadhiwa