• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watuishi |
Mlele District Council
Mlele District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Msingi Mkuu
    • Mpango Mkakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Maji
        • Historia
        • Dhima na Dira
        • Muundo wa Taasisi
        • Ukaribisho
        • Jaribu
        • what we do
        • Huduma ya Maji
        • Huduma za Afya
        • Elimu Msingi
        • Huduma
        • Mwenyekiti wa Halmashauri
        • Mkurugenzi Mtendaji
        • Utawala na Rasilimali watu
        • /TEHAMA-na-Takwimu
        • Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii
        • Mipango takwimu na Ufuatiaji
        • Ardhi na Maliasili
        • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Sheria
        • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
        • Mifugo na Uvuvi
        • Maendeleo ya Jamii
        • Idara
        • Vitengo
        • Ujenzi
        • Maji
        • Ugavi na Manunuzi
        • Usafishaji na Mazingira
        • Uchaguzi
        • Tasaf III
        • Mainstreaming Sustainable Forest Managment in Woodland of Western Tanzania Project
        • Mwenge waUhuru
        • UKIMWI/ VVU
        • Risk Oficer Cordinator
        • Miradi inayoendelea
        • Zabuni
        • Kazi za Idara Utumishi
        • Muundo wa Halmashauri
        • Miradi Lengwa
        • Kitengo cha nyuki
        • Mwenge
        • Sera ya Faragha
        • Kanusho
        • Machapisho
        • Sheria
        • MTF
        • Fomu
        • Orodha ya Madiwani
        • Fedha, Uongozi na Mipango
        • UKIMWI
        • Maji
        • Mipango Miji na Mazingira
        • Uchumi, Afya na Elimu
        • Maadili
        • Ratiba
        • Vikao vya waheshimiwa
        • Kuonana na Mwenyekiti
        • Madiwani
        • Kanausho
        • Huduma ya Maji
        • Huduma ya Afya
        • Huduma ya Kilimo
        • Huduma ya Elimu
        • Huduma ya Ufugaji
        • Huduma za Uvuvi
        • Huduma za Sheria
        • Huduma za kiutumishi
        • Vivutio vya Utalii
        • Kilimo
        • Ufugaji
        • Itakayo tekelezwa
        • Inayoendelea
        • Iliyo Tekelezwa
        • muongozo
        • Sheria Ndogo
        • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
        • Mpango Mkakati
        • Taarifa
        • Fomu Mbalimbali
        • Taarifa kwa Umma
        • Video za shughuli zetu
        • Maktaba ya Picha
        • Magazeti
        • Hotuba
        • ORODHA YA WAJUMBE WA KAMATI MBALIMBALI ZA KUDUMUKWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020
        • KARENDA YA VIKAO VYA KISHERIA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA MLELE KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya
    • Viengo
      • Kitengo cha TEHAMA na Mahusiano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Uchaguzi Uchaguzi
      • Kitengo cha nyuki
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Kilimo na Umwagiliaji
    • Huduma za Kilimo
    • Uvuvi
    • Elimu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orotha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Mazingira
      • UKIMWI
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa
      • Kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayotekelezwa
    • Iliyotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Mkataba wa Huduma
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
  • Kiini cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Album ya Picha
    • Video
    • Hotuba
  • TASAF

miradi ya maendeleo

Posted on: September 22nd, 2022

.Diwani wa Kata ya Ilunde Halmashauri ya Wilaya ya Mhe.Martin Mgoloka upande  akimwongoza Katibu Tawala Mkoa Katavi Bw.Hassan Rugwa kushoto na Afisa Mipango na Ufuatiliaji Halmashauri ya wilaya ya Mlele  Bw.Alfred Sungura wakati wa ukaguzi wa mradi wa nyumba mbili za a waganga kama inavyonekana, iliyojengwa kwa fedha za tozo ambayo ina uwezo wa kukaliwa na familia tatu  nyumba hizo zimejengwa kituo cha Afya Ilunde  nyumba hizo mbili zinathamani ya shilingi milioni 90 fedha za tozo 

Na Kibada Ernest –Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Mlele

HALMASHAURI YA WILAYA YA MLELE KINA CHA   USIMAMIZI WA  MIRADI YA MAENDELEO. 

Utekelezaji wa  Miradi ya  maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele imekuwa chachu ya mabadiliko katika jamii kwa kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.

   Wananchi wametambua umuhimu wa uwepo wa miradi inayotekelezwa katika Halmashauri na kutumia fursa zilizopo katika kujiletea Maendeleo, wanatumia fursa iliyopo ya utekelezaji wa  shughuli za  maendeleo kama ujenzi wa shuleza Msingi na Sekondari.

Ujenzi wa  Zahanati,Vituo vya Afya,Hospitali ya Wilaya,ujenzi wa nyumba za watumishi, miradi ya Maji, miradi ya barabara na shughuli za kilimo.

Shughuli nyingine ni ufugaji,ushirika na uvuvi, biashara na ujasiliamali uhunzi,na nyinginezo zimeongeza  kipato kutokana na uzalishaji mali hali inayofanya wananchi wengi kupata ajira na  wengine kujiari wenyewe kutokana na shughuli kwenye  inayotokana na  miradi hiyo  ya ujenzi, kilimo na shughuli nyingine zinazofanyika katika Halmashauri.

 Ushirikiano huo umefanikisha   kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa kupitia   makusanyo na fedha za mapato ya ndani, fedha kutoka serikali Kuu na Wadau wa Maendeleo   kwa kusimamia vyema ujenzi  na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo ambapo   kwa mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya fedha yenye thamani ya shilingi 7,007,252,388.19  zimetekeleza miradi ya maendeleo kwenye ngazi ya Halmashauri,Kata na Vijiji.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika ukusanyaji wa mapato kwa Halmashauri ya Wilaya  ya Mlele Mhe.Soud Mbogo Mwenyekiti wa Halmashauri   wilaya ya Mlele  anasema katika kipindi cha mwaka wa fedha  2021/2022, amesema moja ya kichocheo cha maendeleo  kwa  halmashauri hiyo ni  vyema katika ukusanyaji wa mapato hali ambayo imesaidia kwa njia moja au nyingine  kubadili maisha ya wananchi

Mhe.Mbogo amesema  Halmashauri ya Wilaya ya Mlele imekusanya shilingi 1, 774,087,421 sawa na asilimia 185 ikivuka lengo lake la mwaka la makusanyo ya Shilingi 957,000,000 katika mwaka wa fedha 2021/2022.

 Hivyo kuwa halmashauri ya pili kitaifa kwa makusanyo nyuma ya Halmashauri ya wilaya ya Kibaha iliyokusanya   kwa asilimia 200 ya lengo ililojiwekea.

 Mafanikio yaliyopatikana katika ukusanyaji wa mapato kwa Halmashauri ya Wilaya  ya Mlele  katika kipindi cha mwaka wa fedha  2021/2022 yameelezwa kuwa ni moja ya kichocheo cha maendeleo  kutokana na halmashauri hiyo kujipanga vyema katika ukusanyaji wa mapato.  

Utekelezaji wa  Miradi ya  maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele imekuwa chachu ya mabadiliko katika jamii kwa kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi kutokana na mabadiliko ya ukuaji wa   Maendeleo kwa wakazi wa  Halmahauri na Wilaya hiyo.

 Wananchi wametambua umuhimu wa uwepo wa miradi inayotekelezwa katika Halmashauri na kutumia fursa zilizopo katika kujiletea Maendeleo, wanatumia fursa iliyopo ya utekelezaji wa  shughuli za  maendeleo kama ujenzi wa shule za Msingi na Sekondari,ujenzi wa  Zahanati,Vituo vya Afya,Hospitali ya Wilaya,ujenzi wa nyumba za watumishi, miradi ya Maji, miradi ya barabara na shughuli za kilimo.

Shughuli nyingine ni ufugaji wa mifugo,ufugaji nyuki,ushirika, na uvuvi, biashara na ujasiliamali uhunzi,na nyinginezo zimeongeza  kipato kutokana na uzalishaji mali hali inayofanya wananchi wengi kupata ajira na  wengine kujiari wenyewe kutokana na shughuli   inayotokana na  miradi hiyo  ya ujenzi.  

 Mhe.Soud Mbogo ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya wilaya ya Mlele anasema anafurahishwa na kasi ya maendeleo  anayoina katika halmashauri yake, hali hii  inatokana mshikamano uliopo kwa  na Viongozi wenzake kuanzia ngazi ya Mkoa ikiongozwa na Mhe. Mwanamvua Mrindoko Mkuu wa Mkoa wa Katavi,

 Mhe.Filberto Sanga, Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe.Isack Kamwelwe Mbunge wa Jimbo la Katavi ilipo Halmashauri ya wilaya ya Mlele, waheshimiwa Madiwani Mkurugenzi Mtendaji  Bi.Teresia Irafay,Timu ya Menejmenti,   watumishi, wadau wote wa Maendeleo na  wananchi  kwa ujumla  jinsi wanavyoshiriki kwa njia moja au nyingine katika kuiletea maendeleo Halmashauri.

Ushirikiano huo umefanikisha   kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa kupitia   makusanyo na fedha za mapato ya ndani, fedha kutoka serikali Kuu na Wadau wa Maendeleo   kwa kusimamia vyema ujenzi  na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika ukusanyaji wa mapato kwa Halmashauri ya Wilaya  ya Mlele  katika kipindi cha mwaka wa fedha  2021/2022 ameeleza kuwa ni moja ni ya kichocheo cha maendeleo ni kutokana na halmashauri hiyo kujipanga vyema katika ukusanyaji wa mapato hali ambayo imesaidia kwa njia moja au nyingine  kubadili maisha ya wananchi

 Kwa mantiki hiyo Halmashauri imefanikiwa kutumia vyema makusanyo hayo na fedha nyingne kutoka serikali Kuu,na wadau wa maendeleo  kwa kusimamia vyema ujenzi  na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo iliyopokea fedha kwa mwaka wa fedha 2021/2022 yenye thamani ya shilingi 7,007,252,388.19 kwenye ngazi ya Halmashauri,Kata na Vijiji.

Miradi yenye jumla ya shilingi 1,211,350,000 inayojumuisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 50,matundu ya vyoo 161 na utengenezaji wa madawati 685 imetekelezwa katika shule za Msingi.

Miradi  yenye jumla ya shilingi 1,643,600,000 inayojumuisha ujenzi wa vyumba 36 vya madarasa, matundu ya vyoo 26,utengenezaji wa madawati 500,ujenzi wa vyumba sita vya maabara za masomo ya sayansi imetekelezwa,pia shule moja ya sekondari Kilinda  na shule nyingine 4 ziko katika hatua za umaliziaji .

Kwa upande wa sekta ya Afya Majengo 19 yamejengwa katika vituo vya Afya na Hospitali ya Wilaya. Huduma ambazo wananchi wa wilaya ya Mlele walikuwa wakisafiri kwenda Sikonge na Mpanda kuzifuata sasa zitatolewa katika Hospitali na Vituo vya Afya vilivyojengwa.

Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 zahanati tatu zimejengwa ambazo ni Kamalampaka,Mlogolo na Mtakuja. Jengo la kuhifadhia maiti na ununuzi wa jokofu katika kituo cha Afya Inyonga B’ vimekamilika. 

Katika sekta ya utawala umaliziaji wa jengo la utawala la Halmashauri ya wilaya ya Mlele unaendelea kusimamiwa na ambapo hadi sasa jengo limekamilika kwa asilimia 95 mwishoni mwa mwezi oktoba halmashauri inategemea kuhamia kwenye ofisi mpya ili kutoa huduma bora kwa wananchi wake.

Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ilibuni na kutekeleza Mradi mpya wa uwepo wa kiwanda cha kufyatua tofali ambao huduma za elimu na afya kufanyika kwa ufanisi,ikizingatiwa ubora wa matofali na muda wa kutekeleza  miradi hiyo.

Jumla ya tofali 140,000 zilifyatuliwa katika kipindi cha mwezi mmoja  na wiki mbili.

Ambapo katika mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri imejipanga kuimarisha miundombinu wezeshi ya kiwanda ili kujiendesha mathalani ununuzi wa lori jipya la halmashauri ili kuhakikisha fadia ya kiwanda inaongezeka na kufanya kuwa chanzo kimojawapo cha mapato ya ndani ya Halmashauri.

Kwa uwepo wa fedha hizo zimesaidia katika kuboresha   huduma za jamii hususani katika sekta ya Afya,elimu,na huduma nyingine  za kijamii kama ujenzi wa  shule za Msingi,sekondari  na zahanati huduma zilizosaidia kupunguza adha iliyokuwa ikiwabili wananchi hapo awali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wameeleza jinsi Jamii inavyonufaika na makusanyo ya fedha za Halmashauri.Miradi mbalimbali ya

    kijamii imeanzishwa inayowanufaisha wananchi kupitia uwezeshwaji wa vikundi hasa  vya wajasiliamali kwa kupatiwa mikopo inayosaidia kuwainua kiuchumi na kuongeza kipato chao kutokana na kuanzisha biashara ndogondogo na shughuli nyingine za uzalishaji mali na viwanda vidogo vidogo vya kiuchumi kama kiwanda cha kutengeneza sabuni, kiwanda cha kukamua alizeti, kiwanda cha karanga na vingievyo.

Mzee Mark Matandiko ni Mkazi wa Inyonga anaeleza moja ya mafanikio yaliyopatikana ni ujenzi wa shule za Msingi na Sekondari,ujenzi wa Zahanati,utoaji wa mikopo kwa akina mama vijana na watu wenye ulemavu ambapo upelekaji wa asilimia kumi umefanikiwa kutokana na ukusanyaji wa mapato ya ndani.

Matandiko anaeleza kuwa mfano Kata ya Inyonga kulikwa na Shule za Msingi mbili Inyonga na Kalovya lakini kwa sasa zimeongezeka shule nyingine mbili na vyumba vya madarasa kuongezwa na kupunguza mrundikano kwa wanafunzi madarasani ujenzi wa shule ya Igombe na Shama ni kutokana na fedha  zilizopatikana kutoka mapato ya ndani.

 Mhe.Leonard Kiyungi ni Diwani wa Kata ya Kamsisi  kwa niaba ya wananchi  anaishukuru serikali kwa jinsi inavyowajari wananchi wake shukurani zimwendee Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa moyo wake wa kuwajari wananchi wa Mlele kwa kuleta fedha kwa ajili ya miradi ya mendeleo kama ujenzi wa shule, Sekta ya Afya,Maji,Barabara na huduma nyingine nyingi za kijamii hivyo kuifanya Mlele kuonekana na kuwa ni moja ya Halmashauri bora hapa nchini.

Ujenzi wa Shule ya Sekondari Kamsisi na Kamalampaka yote ni mafanikio ya hayo yanayoendana na utengenezaji wa madawati hivyo mapato ya ndani yamesaidia kuleta maendeleo yanayoonekana kwa Jamii.

Anasema huu ni ukombozi mkubwa tutumie fursa zilizopo za utekelezaji wa miradi kubadilisha maisha yetu kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kukuza uchumi wa Taifa, Mkoa  Wilaya, Halmashauri na mtu mmoja mmoja ili kuyafikia maendeleo ya kweli.

   Mwisho.

Matangazo

  • TANGAZO KUTOKA TUME HURU YA UCHAGUZI March 03, 2025
  • MABADILIKO YA UKUMBI WA USAILI MLELE DC October 04, 2024
  • Tangazo la Ajira ya ukusanyaji wa Mapato July 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI MBALIMBALI ZA AFYA December 10, 2021
  • Waonaji wote

Habari Mpya

  • MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE SHIKIZI

    April 03, 2025
  • KIKAO CHA WAMILIKI WA VIWANDA VYA KUCHAKATA UNGA

    March 14, 2025
  • MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA TEA KUKABIDHI MIRADI

    February 22, 2025
  • MSAADA WA MADAWATI 136

    January 30, 2025
  • Waonaji wote

Video

#TBC LIVE ZOOM: YALIYOJIRI NA MAFANIKIO YA ZIARA YA RAIS SAMIA NCHINI QATAR
Video Zaidi

wavuti za Haraka

  • FACE BOOK PAGE YA MLELE
  • MLELE DC BLOG
  • kilimo na umwagiliaji
  • mafunzo tovuti za serikali kanda ya magharibi
  • MAONESHO
  • Tuma barua pepe hapa

Wavuti Mwambata

  • Wizara ya Utumishi wa Umma
  • Tume ya ajira ya Tanzania
  • Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania
  • Jamhuri ya muungano wa tanzania
  • Tawala za mikoa na Serikali za mitaa
  • BARAZA LA MITIHANI

Takwimu za Watembeleaji

world map hits counter

Hesabu Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele

    Anuani ya Posta: S.L.P 686 MPANDA

    Simu: +25525295197

    Simu ya Kiganjani: 0786077372

    Barua pepe: ded@mleledc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ya @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Hakizote zimehifadhiwa