MALENGO
. Kuainisha nafasi wazi za viongozi wa vijiji, mitaa, vitongoji na wajumbe waserikali wa vijiji/mitaa na kuwasilisha kwenye mamlaka husika
. Kuratibu chaguzi ndogo za Serikali a Mitaa
. kuandaa ratiba ya uchaguzi na kusambaza kwa vyama vya siasa na wadau wengine
. Kuratibu uteuzi wa wagombea
. Kuratibu uanzishwaji wa maeneo mapya ya kiutawala
. Kuratibu mkutano wa Kwanza wa uchaguzi wa wenyeviti wa Halmashauri mara baada ya uchaguzi mkuu
. Uhakiki endelevu wa vitambulisho vya wapiga kura
. Kutoa elimu ya uchaguzi ya mpigakura
. kutoa matangazo kwa nafasi wazi ya vyama vya siasa
. kutoa mafunzo ya utawala bora kwa viongozi wa serikali za mitaa
Uchaguzi
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 65inaelekeza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ufanyike kila baadaya kipindi cha miaka mitano (5).Kama ilivyo kwa Nchi nyingine Duniani, katika kuendesha shughuli za Uchaguzi,Tanzania hutumia utaratibu wa mzunguko wa Uchaguzi ambao shughuli zakehugawanywa katika awamu tatu (3). Awamu hizo ni shughuli kabla, wakati na baadaya Uchaguzi.Hivyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetekeleza mfumo wa mzunguko wa Uchaguzikwa kufuata awamu hizo Tatu kama ifuatavyo:(a) Kabla ya UchaguziShughuli zilizofanyika katika awamu kabla ya Uchaguzi ni pamoja na:(i) Uandaaji wa Bajeti;(ii) Uandikishaji wa Wapiga Kura;(iii) Ununuzi wa Vifaa;(iv) Uandaaji wa Kalenda na Mpango wa Utekelezaji;(v) Marekebisho ya Sheria na Maelekezo ya Watendaji na Wadau wa Uchaguzi;(vi) Mafunzo kwa Watendaji wa Uchaguzi;(vii) Kutoa Elimu ya Mpiga Kura; na(b) Wakati wa UchaguziKatika awamu hii, Tume ilifanya shughuli zifuatazo:(i) Uteuzi wa Wagombea;(ii) Uratibu wa Kampeni za Wagombea;55(iii) Utekelezaji wa Kamati za Maadili;(iv) Usajili wa Watazamaji wa Uchaguzi.(v) Kuchapa na kusambaza Karatasi za Kura;(vi) Kusambaza Vifaa vya Uchaguzi;Upigaji Kura;(vii) Kuhesabu Kura; na(viii) Kutangaza Matokeo.(c) Baada ya UchaguziKatika awamu hii, Tume inafanya shughuli zifuatazo:(i) Tathmini baada ya Uchaguzi Mkuu;(ii) Kushughulikia Kesi za Uchaguzi; na(iii) Kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu.(iv) Marekebisho ya Sheria za Uchaguzi;(v) Kupitia na kuboresha Daftari la Wapiga Kura;(vi) Kupitia na kuboresha Mifumo ya Uchaguzi;(vii) Kupitia na kuboresha mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi;(viii) Kupitia na kuboresha Muundo wa Tume;(ix) Ukaguzi wa matumizi ya fedha na vifaa vilivyotumika katika Uchaguzi Mkuu;(x) Kupitia Mpango Mkakati; na(xi) Kuandaa Mpango Kazi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu unaofuata.
Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
Anuani ya Posta: S.L.P 686 MPANDA
Simu: +255759023788
Simu ya Kiganjani: 0759023788
Barua pepe: ded@mleledc.go.tz
Hakimiliki ya @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Hakizote zimehifadhiwa